-
Wabunge wa CHADEMA waliojitenga na watu kwa sababu ya Corona wamerejea leo bungeni
May 15, 2020 10:29Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA nchini Tanzania kimetoa taarifa kikisema kuwa, wabunge wote wa Chama hicho ambao hatimae wamehitimisha siku 14 za kujiweka karantini kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli za bunge, pamoja na vikao vya bunge au kufika ndani ya ukumbi na kamati zake katika maeneo mengine ya mhimili huo, leo Ijumaa, wamerejea bungeni kuendelea na majukumu yao, baada ya kuwa na uhakika kuwa hawana maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19, unaosababishwa na virusi vya Corona.
-
Rais Magufuli awataka Watanzania wachape kazi licha ya maambukizi ya corona
May 03, 2020 06:50Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amewataka wananchi wa nchi hiyo wasiwe na hofu yoyote ya corona na waendelee kuchapa kazi kama kawaida.
-
Vifo vya Corona nchini Tanzania vyafikia 16, maabukizi yakaribia 500
Apr 29, 2020 06:58Idadi ya watu walioaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 (Corona) nchini Tanzania imeongezeka na kufikia watu 16.
-
Kampeni za uchaguzi mkuu kuanza kesho Jumatatu nchini Burundi
Apr 26, 2020 07:05Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametia saini rasmi amri ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu wa rais bunge na madiwani nchini humo. Kampeni hizo zitaanza kesho Jumatatu na kuendelea hadi Jumapili ya tarehe 17 mwezi ujao wa Mei.
-
Baada ya kuongezeka wagonjwa 23, idadi ya walioambukizwa virusi vya corona Zanzibar yafikia 58
Apr 19, 2020 10:31Wizara ya Afya ya Zanzibar imetangaza wagonjwa wapya 23 wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona vya COVID-19.
-
Watu 18 waaga dunia katika ajali ya barabarani Tanzania
Apr 15, 2020 03:46Watu 18 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, mashariki mwa Tanzania.
-
Wagonjwa wapya 14 wa COVID-19 wabainika nchini Tanzania
Apr 13, 2020 03:41Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema kuwa, watu 14 ambao wote ni raia wa Tanzania wamepatikana na ugonjwa wa corona na kufanya idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 nchini humo kufikia 46.
-
Hatimaye corona yailazimisha Tanzania kupiga marufu safari za ndege, Marekani yaongoza kwa vifo na maambukizi
Apr 12, 2020 23:16Hatimaye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga marufuku safari zote za ndege za abiria za kimataifa ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo kusisitizia msimamo wake wa kutofunga mipaka ya Tanzania akisema kuwa kufunga mipaka hiyo kutaziletea madhara makubwa nchi jirani kama za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Magufuli: Mlipuko wa corona hautafanya uchaguzi mkuu wa Tanzania uakhirishwe
Mar 26, 2020 08:47Rais John Magufuli wa Tanzania amesema uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautaakhirishwa licha ya kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona.
-
Watu 27 waliochukuliwa sampuli ya vipimo vya Corona Tanzania, wako salama
Mar 19, 2020 13:02Watu 27 ambao walichukuliwa sampuli za vipimo vya afya ili kuwachunguza iwapo wameambukizwa virusi vya Corona Covid-19, wapo salama.