-
Indhari kuhusu kurejea udikteta huko Tunisia
Dec 30, 2021 11:36Rached Ghannouchi Spika wa Bunge lililosimamishwa la Tunisia amezitaja hatua na maamuzi yanayochukuliwa na Rais wa nchi hiyo, Kais Saied kuwa ni sawa ni kuhuisha tajiriba iliyofeli na kueleza kuwa, Tunisia inaelekea katika mkondo wa kurejea kwenye udikteta na kutengwa.
-
Kongamano la kumuenzi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes lafanyika Tunisia
Dec 30, 2021 08:17Kundi la vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini Tunisia zimefanya kongamano kwa mnasaba wa mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi.
-
Marzouki ajibu mapigo, asema hukumu dhidi yake haina maana, imetolewa na rais asiye halali
Dec 24, 2021 02:50Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki amesema kuwa tuhuma zote zinazomkabili zimepindua uhakika wa mambo na zinamhusu Rais Kais Saied mwenyewe. Al Marzouki ametoa matamshi hayo akizungumzia hukumu ya awali iliyotolewa dhidi yake na mahakama nchini Tunisia bila ya kuwepo mahakamani, na kumhukumu kifungo cha miaka 4 jela.
-
Rais wa zamani wa Tunisia ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumpinga rais
Dec 23, 2021 07:12Mahakama ya Tunisia imemhukumu rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Moncef Marzouki kifungo cha miaka minne jela.
-
Mwanasheria wa Tunisia awasilisha mashtaka ya "uhaini mkubwa" dhidi ya Kais Saied, Al Sisi na mrithi wa utawala wa Imarati
Dec 23, 2021 02:51Mwanasheria wa Tunisia ametangaza kuwa amefungua kesi mahakamani dhidi ya baadhi ya maafisa wa serikali ya Tunisia na baadi ya viongozi wa Kiarabu kwa tuhuma za "uhaini mkubwa".
-
Tume ya Uchaguzi Tunisia: Rais Saied hakushauriana nasi kuhusu kura ya maoni au uchaguzi
Dec 16, 2021 16:40Adel Brinsi ambaye ni mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tunisia, amesema kuwa Rais Kais Saied wa nchi hiyo hakushauriana na mamlaka hiyo kuhusu suala la kuitisha kura ya maoni ya marekebisho ya Katiba au uchaguzi ujao wa Bunge uliopangwa kufanyika Disemba 17 mwaka ujao.
-
Rais wa Tunisia: Bunge linaendelea kusitishwa hadi uchaguzi mpya utakapoandaliwa
Dec 14, 2021 03:23Rais wa Tunisia Kais Saied alitangaza jioni ya Jumatatu jana kwamba Bunge la nchi hiyo litaendelea kusitishwa hadi uchaguzi mpya utakapoandaliwa, akiyashutumu makundi ya kisiasa kuwa yamesaliti nchi na kupora fedha za umma.
-
Mabrouk: Tunisia sasa iko nje ya klabu ya mataifa ya kidemokrasia
Dec 11, 2021 08:09Waziri wa zamani wa Tunisia ameseaa kuwa nchi hiyo imeachana na klabu ya nchi za kidemokrasia baada ya rais wa nchi hiyo kutwaa mamlaka yote ya utendaji mapema mwaka huu, na kusababisha mzozo mkubwa wa kisiasa nchini humo.
-
Kuendelea mgogoro wa kisiasa Tunisia
Dec 03, 2021 04:33Licha ya mgogoro wa kisiasa wa Tunisia kuendela kwa miezi kadhaa sambamba na kufanyika juhudi za kujaribu kuumaliza, lakini juhudi hizo zimeshindwa kuzaa matunda.
-
Financial Times: Fungate ya Rais Kais Saied wa Tunisia inaelekea ukingoni
Nov 16, 2021 07:09Gazeti la Financial Time la Uingereza limeripoti kuwa wataalamu wanasema fungate ya Rais wa Tunisia itamalizika hivi karibuni kutokana na mashaka ya kushindwa kwake kupata suluhisho la haraka la mgogoro wa kiuchumi unaoisumbua nchi hiyo licha ya kuwa na uungaji mkono wa kiasi fulani kwa sasa.