-
Kuendelea chuki za rais wa Ufaransa dhidi ya Uislamu
Nov 23, 2020 01:04Ikiwa ni kuendeleza chuki zake dhidi ya Uislamu na Waislamu, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, sasa ametoa muhula maalumu kwa viongozi wa makundi ya Kiislamu ya nchi hiyo kuhakikisha wanajivika utamaduni wa Magharibi hata katika mambo ambayo ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
-
Erdogan: Dunia ipige vita uadui dhidi ya Uislamu sawa ilivyo katika suala la kupiga vita Uyahudi
Nov 03, 2020 02:45Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ameitaka dunia ijifunze na kupata somo na ibra kutokana na uzembe wa jamii ya kimataifa iliyoacha kuzuia mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Bosnia Herzegovina na kusisitiza kuwa, dunia inapaswa kupiga marufuku na kupambana na chuki na uhasama dhidi ya Uislamu kama ilivyopambana na chuki dhidi ya Uyahudi baada ya Holocaust (yanayodaiwa kuwa mauaji ya Mayahudi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia).
-
Waziri Mkuu wa Canada apingana na Macron, asema Uislamu hauna mfungamano na ugaidi
Oct 30, 2020 08:54Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema kuwa gaidi aliyetekeleza hujuma ya kigaidi katika mji wa Nice nchini Ufaransa hawakilishi dini ya Uislamu wala Waislamu, na kwamba watu wote wanapasa kukiri ukweli huo.
-
Radiamali ya kindumakuwili ya Ufaransa kufuatia malalamiko ya Waislamu duniani
Oct 28, 2020 07:41Waislamu duniani kote wamekasirishwa na kushadidi vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa hasa cha kuchapishwa tena katuni zinazomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW. Hasira za Waislamu zimeongezeka maradufu baada ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kutetea vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu kwa kisingizo cha uhuru wa maoni.
-
Pogba 'ajiuzulu' timu ya taifa ya Ufaransa kufuatia matamshi ya Macron dhidi ya Uislamu
Oct 26, 2020 11:51Mchezaji nyota wa soka, Paul Pogba ameripotiwa kujiuzulu katika timu ya taifa ya soka ya Ufaransa, kutokana na matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo ya Ulaya dhidi ya Uislamu, wakati akitetea vitendo vya kutusiwa na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (SAW).
-
Erdogan: Rais wa Ufaransa apimwe uwezo wake wa kiakili baada ya matamshi yake dhidi ya Waislamu
Oct 25, 2020 12:51Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa Rais wa Ufaransa, Emanue Macron, anahitaji kupimwa uwezo wake wa kiakili baada ya matamshi ya kibaguzi aliyotoa karibuni kuhusu dini ya Uislamu.
-
Waislamu wa Ufaransa wamjia juu Macron kwa matamshi yake dhidi ya Uislamu
Oct 07, 2020 07:56Waislamu nchini Ufaransa wamekosoa vikali kauli ya Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kuhusu Uislamu na kusisitiza kuwa, matamshi ya rais huyo ni ya kibaguzi.
-
Rais Rouhani: Waislamu wasimame kidete kutetea na kulinda thamani za Uislamu
Sep 11, 2020 04:46Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani kitendo cha jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, ameyataka mataifa ya Kiislamu kusimama kidete kutetea na kulinda thamani, utamaduni na matukufu ya dini yao.
-
Pakistan yasikitishwa na Charlie Hebdo kumvunjia tena heshima Mtume SAW
Sep 02, 2020 07:57Pakistan imelaani vikali uamuzi wa jarida linalochapishwa nchini Ufaransa la Charlie Hebdo wa kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW).
-
Rais wa Tunisia: Msingi wa mirathi katika Uislamu ni uadilifu na insafu
Aug 17, 2020 07:38Rais Kais Saied wa Tunisia ameamsha hasira za jumuiya za wanawake za kiliberali baada ya kusisitiza kwamba msingi wa mirathi katika dini ya Uislamu ni uadilifu na insafu na kwamba suala hilo limeshapewa ufumbuzi katika aya za Qu'ani tukufu ambao hauhitajii tena tafsiri wala taawili.