-
Mazungumzo ya Istanbul na sisitizo la uanachama wa Ukraine katika Umoja wa Ulaya
Mar 30, 2022 21:58Duru mpya ya mazungumzo kati ya wajumbe wa Russia na Ukraine ilifanyika mjini Istanbul, Uturuki siku ya Jumanne iliyopita. Baada ya mazungumzo na Russia, mkuu wa ujumbe wa Ukraine, David Arakhamia, alisema kuwa hakuna mtu anayeweza kuizuia Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya.
-
Mkuu wa Benki ya Maendeleo Afrika: Vita vya Ukraine vinaweza kusababisha mgogoro wa chakula Afrika
Mar 29, 2022 22:30Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) ambayo ni mkopeshaji mkubwa barani humo anafanya kila awezalo kuzuia bara la Afrika lisikabiliwa na mgogoro wa chakula kutokana na athari mbaya za vita vya Rusia na Ukraine.
-
Uingereza kuipa Ukraine makombora ya kutungulia ndege kukabiliana na Russia
Mar 28, 2022 02:47Waziri wa Ulinzi wa Uingereza ametangaza kuwa London imeamua kuipa Ukraine makombora ya kutungulia ndege ili kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Russia.
-
Russia: Ukraine imegeuzwa kimbilio la magaidi na mamluki wa kimataifa
Mar 27, 2022 06:01Wizara ya Ulinzi ya Russia imeashiria kufanikiwa malengo ya operesheni ya kijeshi ya nchi hiyo nchini Ukraine kwa asilimia kubwa na kufichua kuwa, maelfu ya magaidi na mamluki wa nchi ajinabi wamekimbilia katika nchi hiyo ya Ulaya mashariki.
-
Russia: Marekani itoe maelezo kuhusu nafasi ya mtoto wa Biden katika maabara za silaha za kibaolojia huko Ukraine
Mar 25, 2022 22:34Russia imetaka ipewe maelezo kutoka kwa Marekani kuhusu jukumu la mtoto wa Rais Joe Biden wa nchi hiyo katika maabara za kibaolojia nchini Ukraine.
-
Kikao cha wakuu wa NATO na kung'ang'ania msimamo wa kiuadui dhidi ya Russia
Mar 25, 2022 21:52Kikao cha dharura cha wakuu wa Jeshi la Nchi za Magharibi NATO kilifanyika juzi Alkhamisi mjini Brussels, Ubelgiji ambayo ndio makao makuu ya Umoja wa Ulaya. Katika siku za hivi karibuni, Brussels imekuwa mwenyeji wa vikao vitatu ambavyo ni cha wakuu wa NATO, cha G7 na cha Umoja wa Ulaya.
-
Vita vya Ukraine na mgogoro wa chakula duniani
Mar 24, 2022 21:57Zaidi ya nchi 40 zimetia saini barua ya kutaka kuitishwe mkutano wa dharura wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ili kukabiliana na mgogoro wa chakula, ambao huenda ukazidishwa na vita vya Ukraine.
-
Kremlin: Russia itatumia silaha za nyuklia uwepo wake ukitishiwa
Mar 23, 2022 07:18Ikulu ya Russia ya Kremlin imesema nchi hiyo haitakuwa na chaguo jingine isipokuwa kutumia silaha za nyuklia iwapo uwepo wa taifa hilo utakabiliwa na vitisho.
-
Russia yajibu madai ya Biden ya matumizi ya silaha za kibaolojia nchini Ukraine
Mar 22, 2022 08:24Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Ryabkov amesema Jumanne leo kwamba matamshi yaliyotolewa na Rais wa Marekani, Joe Biden kuhusu uwezekano wa Russia kutumia silaha za kemikali na za kibaolojia huko Ukraine ni ya kihabithi.
-
Shutuma za Russia kwa Marekani inayokwamisha mazungumzo ya Ukraine
Mar 21, 2022 22:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergeĭ Viktorovich Lavrov ameishutumu vikali Marekani kwa siasa zake kuhusu vita vya Ukraine na kusema kuwa, Washington ndiyo inayokwamisha kufikiwa makubaliano baina ya Moscow na Kyiv hata katika masuala madogo kabisa. Amesema, hivi sasa Marekani inawatwisha viongozi wa Ukraine misimamo yake na ndio maana Kyiv inakwamisha kila kitu katika mazungumzo yake na Russia.