Russia: Ukraine imegeuzwa kimbilio la magaidi na mamluki wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i81842-russia_ukraine_imegeuzwa_kimbilio_la_magaidi_na_mamluki_wa_kimataifa
Wizara ya Ulinzi ya Russia imeashiria kufanikiwa malengo ya operesheni ya kijeshi ya nchi hiyo nchini Ukraine kwa asilimia kubwa na kufichua kuwa, maelfu ya magaidi na mamluki wa nchi ajinabi wamekimbilia katika nchi hiyo ya Ulaya mashariki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 27, 2022 06:01 UTC
  • Russia: Ukraine imegeuzwa kimbilio la magaidi na mamluki wa kimataifa

Wizara ya Ulinzi ya Russia imeashiria kufanikiwa malengo ya operesheni ya kijeshi ya nchi hiyo nchini Ukraine kwa asilimia kubwa na kufichua kuwa, maelfu ya magaidi na mamluki wa nchi ajinabi wamekimbilia katika nchi hiyo ya Ulaya mashariki.

Meja Jenerali Igor Yevgenyevich Konashenkov, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema Ukraine imepokea magaidi na mamluki 6,595 kutoka nchi 62 duniani, lakini hakuna shaka kuwa vikosi vya Russia vitawaangamiza wote.

Amesisitiza kuwa, katika marhala ya kwanza ya operesheni maalumu ya kijeshi ya Russia, nchi hiyo imefanikiwa kusambaratisha karibu mfumo mzima wa ulinzi wa anga na bahari wa Ukraine.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia ameongeza kuwa, Wamagharibi wamefanya makosa makubwa kwa kuipa Ukraine silaha na zana za kivita, jambo ambalo linarefusha mgogoro wa Ukraine.

Meja Jenerali Igor Yevgenyevich Konashenkov, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia

Mapema mwezi huu, Idara ya Ujasusi wa Nje ya Russia (SVR) ilionya kwamba, Marekani inawapa mafunzo magaidi wa Daesh (ISIS) katika kituo cha Al-Tanf nchini Syria ili wapelekwe Ukraine.

Idara hiyo ilifichua kuwa, Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na Kamandi ya Operesheni Maalumu ya Marekani inaendelea kuunda vitengo vipya vya Daesh Magharibi mwa Asia na nchi za Afrika na imepangwa kuwa, magaidi hao watapelekwa Ukraine kwa kushirikiana na mashirika ya ujasusi ya nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO.