-
UN yalaani hatua ya Israel ya kuendelea kuua watoto wa Kipalestina
Dec 18, 2020 03:50Wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali kitendo cha wanajeshi wa utawala haramu wa Israel cha kumuua kijana mwingine wa Kipalestina, huo ukiwa ni muendelezo wa mauaji dhidi ya watoto wa Kipalestina yanayofanywa na Wazayuni.
-
UN yatiwa wasiwasi na mapigano Msumbiji; laki 4 wahama makazi yao
Dec 14, 2020 08:52Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, mgogoro mkubwa wa kibinadamu unanukia kaskazini mwa Msumbiji, ambapo watu zaidi ya laki nne wamelazimika kuyahama makazi yao wakihofia usalama wao.
-
UN yailaumu Marekani kwa msimamo wake kuhusu Sahara Magharibi
Dec 13, 2020 04:06Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameilaumu Marekani kwa kutangaza kulitambua rasmi eneo la Sahara Magharibi kuwa ni milki ya Morocco.
-
UN yatoa indhari: Hali ya dharura ya mabadiliko ya tabianchi inahitaji hatua za haraka
Dec 12, 2020 22:17Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa dunia hivi sasa inakabuliwa na hali ya dharura ya mabadiliko ya tabianchi.
-
Hatua mpya ya utatuzi wa mgogoro wa Libya; maafikiano kuhusu namna ya kuwachagua viongozi wakuu wa serikali
Dec 09, 2020 09:24Awamu muhimu ya vita vya ndani vya Libya ilianza kwa shambulio la mwezi Aprili 2019 lililofanywa na kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na Khalifa Haftar ambalo shabaha yake ilikuwa ni kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na kuiangusha Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa (GNA); na wigo wa vita hivyo ukapanuka zaidi kwa uingiliaji wa pande za kigeni zinazounga mkono mirengo miwili hiyo.
-
UN yapitisha azimio kuitaka Israel iachane na mpango wa kumiliki silaha za atomiki
Dec 08, 2020 23:06Umoja wa Mataifa umepitisha azimio lenye anuani "hatari ya kuenea silaha za nyuklia Asia Magharibi" na kuutaka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel uachane na mpango wa kumiliki silaha za atomiki.
-
Ombi kwa Biden kwa ajili ya kuhitimisha ushiriki wa Marekani katika vita vya Yemen
Dec 05, 2020 21:13Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zina nafasi muhimu katika vita huko Yemen ambavyo viilanzishwa tangu mwezi Machi mwaka 2015 na muungano vamizi chini ya uongozi wa Saudi Arabia kutokana na hatua yao ya kuzipatia Saudia na Imarati misaada mbalimbali ya kilojistiki, kiintelijensia na kijeshi. Kitendo hicho kimekosolewa vikali na jumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu.
-
Mjumbe wa UN: Libya ina "hali mbaya sana" kwa kuendelea kuwepo wapiganaji 20,000 wa kigeni
Dec 03, 2020 03:59Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametahadharisha kuwa, kuwepo wapiganaji na mamluki wasiopungua 20,000 wa kigeni nchini humo kunaifanya "hali iwe mbaya sana" huku silaha zikiendelea kumiminika pia katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini iliyoharibiwa vibaya na vita.
-
Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa mivutano huko al Hudaydah, Yemen
Dec 01, 2020 00:54Mkuu wa Timu ya Uangalizi ya Umoja wa Mataifa huko Yemen ametaka kutekelezwa usitishaji vita katika mji wa al Hudaydah magharibi mwa nchi hiyo sambamba na kusitishwa mivutano katika eneo hilo.
-
Burundi yataka kufungwa ofisi ya mjumbe maalumu wa UN nchini humo
Nov 20, 2020 23:14Serikali ya Burundi imesema haikaribishi tena kuwepo na Ofisi ya Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, na kwamba taifa hilo lina amani baada ya kushuhudia mgogoro wa kisiasa kwa miaka kadhaa.