-
Kupamba moto mgogoro wa wakimbizi barani Ulaya
Nov 11, 2021 07:10Kwa mara nyingine tena, wimbi la wakimbizi wanaomiminika kwenye mipaka ya nchi za Ulaya limeongezeka na kuwa mgogoro mkubwa. Nchi za Ulaya zimeamua kufunga mipaka yao ili kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wapya.
-
Mtaalamu wa WHO: Ulaya inaweza kukumbwa na vifo vingine vya corona laki tano
Nov 04, 2021 20:25Kiwango cha sasa cha maambukizi ya corona barani Ulaya kinatia wasiwasi mkubwa na bara hilo linaweza kukumbwa na vifo vingine laki tano vya corona ifikapo mapema mwakani. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya.
-
Kukosoa Uturuki utendaji wa Umoja wa Ulaya ulio dhidi ya Uislamu
Nov 04, 2021 20:23Ukosoaji mtawalia wa viongozi wa Uturuki dhidi ya Umoja wa Ulaya hususan sera za chuki dhidi ya Uislamu za umoja huo, zinapaswa kutathminiwa kama juhudi za Ankara za kukabiliana na sera za madola ya Magharibi dhidi ya serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan na kuimarisha wenzo wa kuishinikiza jumuiya hiyo ya Ulaya.
-
Madai ya Ufaransa kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran, kuendelezwa sera za kindumakuwili za Ulaya
Oct 23, 2021 22:55Sambamba na mkutano wa Ijumaa ya wiki hii baina ya wawakilishi wa Marekani na nchi za Ulaya uliofanyika mjini Paris, Ufaransa imeitaka Iran ipunguze shughuli zake za kuzalisha nishati ya nyuklia.
-
Ungamo la Josep Borrell la kupungua ushawishi wa Umoja wa Ulaya
Oct 12, 2021 08:32Hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuifuata kibubusa Marekani imeitilia alama ya swali utendaji na mamlaka ya uchukuaji maamuzi ya umoja huo katika medani za kimataifa.
-
Umoja wa Ulaya wafuta makubaliano yake ya biashara na Morocco
Sep 30, 2021 02:56Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya imefuta makubaliano ya biashara baina ya nchi za umoja huo na Morocco kutokana na mgogoro wa Polisario.
-
Mgogoro wa nishati Uingereza, nembo ya kushindwa serikali ya Wahafidhina
Sep 29, 2021 22:53Mgogoro wa mafuta na uhaba wa petroli nchini Uingereza ni mkubwa kisasi kwamba magari yamekuwa yakihujumu vituo vya mafuta kwa ajili ya kupata bidhaa hiyo muhimu lakini bila mafanikio, jambo ambalo hatimaye limeipelekea serikali ya Wahafidhina kulitaka jeshi liwe tayari kuingilia kati ili kuokoa hali ya mambo.
-
Juhudi za Biden za kujaribu kupunguza mvutano baina ya Marekani na Ufaransa
Sep 23, 2021 22:46Kufuatia mazungumzo ya simu ya Marais Joe Biden wa Marekani na Emmanuel Macron wa Ufaransa hapo siku ya Jumatano, viongozi hao wametoa taarifa ya pamoja wakisema wameamua kuendelea na mashauriano kwa ajili ya kutatua hitilifu zilizojitokeza baina ya pande mbili kuhusu mkataba wa kiusalama wa AUKUS.
-
Mawaziri wa EU waiunga mkono Ufaransa dhidi ya Marekani katika mzozo wa nyambizi
Sep 21, 2021 03:10Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Joseph Borrell amesema nchi wanachama wa umoja huo zimeonyesha uungaji mkono wao na mshikamano kwa Ufaransa katika mzozo wa nyambizi kati yake na Marekani.
-
Kushadidi mivutano baina ya Marekani na Ufaransa, Paris yamwita nyumbani balozi wake mjini Washington
Sep 18, 2021 21:52Ufaransa imechukua uamuzi wa kumwita nyumbani balozi wake mjini Washington sambamba na kushadidi mivutano katika uhusiano wa serikali ya Paris na Marekani. Vilevile imechukua hatua ya kumrejesha nyumbani balozi wake nchini Australia kama hatua ya kuonesha malalamiko yake.