Sep 30, 2021 06:26 UTC
  • Donald Trump aliirubuni Morocco itangaze uhusiano wa kawaida na Wazayuni na isaliti malengo matukufu ya Palestina
    Donald Trump aliirubuni Morocco itangaze uhusiano wa kawaida na Wazayuni na isaliti malengo matukufu ya Palestina

Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya imefuta makubaliano ya biashara baina ya nchi za umoja huo na Morocco kutokana na mgogoro wa Polisario.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mahakam hiyo ya Umoja wa Ulaya yenye makao yake nchini Luxembourg imetoa hukumu hiyo baada ya taasisi ya kisiasa na kijeshi ya Polisario kufungua mashtaka dhidi ya Morocco kuhusu makubaliano mawili ya kilimo na uvuvi katika fukwe za Sahara Magharibi yaliyokuwa yamefikiwa baina ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Morocco.

Serikali ya Morocco iliamua kuisaliti kadhia ya Palestina na kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel baada ya Marekani kusema italitambua eneo la Sahara Magharibi kuwa ni mali ya Morocco. 

Wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi wa Sahama Magharibi (Polisario)

 

Nchi hiyo ya Kiarabu ilikuwa na tamaa pia kwamba Umoja wa Ulaya nao utafuata mkumbo na utaweka mikataba ya kila namna na Rabbat baada ya usaliti wake huo kwa suala la Palestina. Hata hivyo mwaka mmoja tu baada ya kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala katili wa Kizayuni unaofanya jinai za kila namna dhidi ya Wapalestina, Umoja wa Ulaya umeamua kufuta makulibano yake ya kibiashara na Morocco suala ambalo ni pigo kubwa kwa sekta ya kiuchumi ya nchi hiyo ya kaskazini magharibi mwa Afrika.

Wakati wa urais wa Donald Trump huko Marekani, rais huyo Mzayuni mwenye chuki na Uislamu na Waislamu wakiwemo Wapalestina, aliirubuni Morocco kuwa mambo yake yatatengenea iwapo itasaliti malengo matukufu ya Palesitna na kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tags