May 07, 2024 06:36 UTC
  • Borrell: EU na Jamii ya Kimataifa zinapaswa kuzuia uvamizi na mashambulio ya Israel Rafah

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema, amri iliyotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwataka wakazi wa mashariki ya Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza wahame katika eneo hilo haikubaliki.

Joseph Borrell ameeleza hayo kwenye ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambapo sambamba na kusisitiza kuwa utawala wa Israel unapaswa uachane na mpango wa kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Rafah, amesema Umoja wa Ulaya na Jamii ya Kimataifa zinapaswa kuzuia uvamizi na mashambulizi ya utawala wa Israel mfanyamauaji ya kimbari.
Hali ya Wapalestina walioko Rafah waliopoteza makazi yao katika maeneo mengine ya Ghaza

Jeshi la Kizayuni limetangaza kuwa, wakazi wa mashariki mwa Rafah wanapaswa kuuhama haraka sana mji huo na kuhamia kwenye lilichokiita eneo "pana la huduma za kibinadamu" la al-Mawasi huko Khan Yunis ili operesheni ya ardhini ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah ipate kuanza.

 
Jeshi la Kizayuni limeeleza pia kwamba, operesheni ya kuwahamisha Wapalestina eneo la Rafah Mashariki inajumuisha watu wapatao 100,000 na ni sehemu ya oparesheni ndogo, na kwamba halitabainisha utaratibu wa muda wa kuwahamisha watu katika eneo hilo mpaka litakapokamilisha kufanya tathmini ya operesheni hiyo.../

 

Tags