-
Baraza la Makanisa Duniani lataka kuwekewa vikwazo Israel kutokana na vita vya Gaza
Jan 01, 2026 23:18Baraza la Makanisa Duniani (WCC) limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kuiwekea Israel vikwazo vikiwemo vya silaha kutokana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza, na ukiukaji wa haki dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
WHO: Unywaji wa pombe unaua watu 800,000 kila mwaka Ulaya
Dec 28, 2025 03:05Unywaji wa pombe unasababisha vifo vya watu zaidi ya 800,000 kila mwaka barani Ulaya, na kusababisha kifo kimoja kati ya kila vifo kumi na moja, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO).
-
Nchi 14 zikiwemo za EU zalaani mpango wa ujenzi haramu Ukingo wa Magharibi
Dec 25, 2025 03:10Kundi la nchi 14 zikiwemo za Ulaya limetoa taarifa ya pamoja ya kulaani vikali uamuzi wa Israel wa kuanzisha ujenzi mpya wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu, na kuitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
-
Sambamba na kuanza tena chokochoko za Trump, EU yasema iko pamoja na Denmark, Greenland
Dec 23, 2025 07:48Umoja wa Ulaya umeonyesha mshikamano na Denmark na eneo la Greenland kufuatia tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuteua mjumbe wake maalumu katika eneo hilo.
-
Kikao cha Brussels na kurudi nyuma Ulaya inayosokotwa na tofauti za ndani, katika mpango wake wa unyang'anyi wa mali za Russia
Dec 20, 2025 23:09Licha ya viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuandamwa na mashinikizo ya kisiasa ya Marekani ya kuwataka watoe msukumo wa kuvipatia suluhisho la haraka vita vya Ukraine, viongozi hao waliokutana kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Brussels, wameamua kurudi nyuma na kulegeza msimamo katika uchukuaji uamuzi wenye gharama kubwa na hasi wa kunyakua mali za Russia,
-
Kwa nini EU imejikita katika kuwafukuza wakimbizi badala ya kutatua mgogoro wa uhamiaji?
Dec 12, 2025 23:01Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) zimeidhinisha rasimu ya "Kanuni ya kuanzisha mfumo wa pamoja wa kuwarejesha raia wa nchi ya tatu wasio na vibali halali vya ukaazi.
-
Karibu 50% ya raia wa nchi wananchama wa EU wanamuona Trump "adui wa Ulaya"
Dec 05, 2025 03:03Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni umebaini kuwa, karibu nusu ya raia wa nchi wananchama wa Umoja wa Ulaya, EU wanamwona Rais wa Marekani Donald Trump kama "adui wa Ulaya," huku wengi miongoni mwao wakihisi hatari ya kuzuka vita vya wazi baina ya nchi zao na Russia katika miaka ijayo kuwa ni ya "juu".
-
Baraza la Waislamu Ufaransa latoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu ujasusi dhidi ya Waislamu kwa niaba ya Israel
Nov 28, 2025 23:54Baraza la Waislamu la Ufaransa limetoa wito kwa serikali kuanzisha uchunguzi kuhusu madai kwamba watu wawili walikusanya taarifa kuhusu Waislamu nchini Ufaransa na kuzikabidhi kwa shirika la ujasusi la Israel.
-
Mahakama ya EU yaiamuru nchi mwanachama itambue 'ndoa' za jinsia moja
Nov 26, 2025 07:20Mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Ulaya imetoa hukumu kwamba Poland inalazimika kuzitambua ndoa za jinsia moja zilizosajiliwa katika nchi zingine wanachama wa umoja huo japokuwa mahusiano kama hayo yako kinyume cha sheria kulingana na sheria za kitaifa za nchi hiyo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani: EU siyo inayoainisha sheria za kimataifa
Nov 14, 2025 04:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema, nchi yake haitakubali mahubiri yanayotolewa na Umoja wa Ulaya EU kuhusu jinsi inavyoendesha shughuli zake za usalama wa taifa na akapuuza ukosoaji wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa mashambulizi ya kijeshi yanayofanywa na Marekani kuzilenga boti zinazopita eneo la Carribean.