Kansela wa Ujerumani akiri kuhitilafiana Umoja wa Ulaya kuhusu Ukraine
Kansela wa Ujerumani amesema kuwa anahitilafiana pakubwa kimitazamo na Waziri Mkuu wa Hungary kuhusu namna ya kushughulikia mgogoro wa Ukraine na kukiri kuwepo hitilafu hizo ndani ya Umoja wa Ulaya kuhusu Ukraine.
Olaf Scholz ameashiria namna ambavyo wanachama wote wa Umoja wa Ulaya hawaungi mkono msimamo maalumu kuhusu mgogoro wa Ukraine na kusema: Mitazamo ya Viktor Orban, Waziri Mkuu wa Hungary, kuhusu vita vya Ukraine inatofautiana na maoni ya viongozi wengi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Viktor Orban amekuwa akikosoa uungaji mkono wa EU kwa Ukraine na kutoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano kati ya Moscow na Kyiv. Waziri Mkuu wa Hungary aidha amelaani vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia.
Russia ilianzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya maeneo ya Luhansk na Donetsk Februari 24 mwaka 2022 baada ya kutambua rasmi kujitenga maeneo hayo na Ukraine.
Moscow ilitangaza kuwa lengo la hatua hiyo ni kuiondoa Ukraine katika mikono ya manazi, kuipokonya silaha nchi hiyo, kutatua masuala yake ya usalama na kujibu ombi la msaada la watu wa Luhansk na Donetsk.