-
Kwa nini maandamano ya kupinga kuungwa mkono Israel yameongezeka barani Ulaya?
Sep 15, 2025 07:30Maelfu ya watu wamemiminika barabarani mjini Berlin kupinga sera za Ujerumani katika eneo la Asia Magharibi hususan za kuunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais wa zamani wa Ireland: Nikiwa raia wa Ulaya 'naona aibu' kwa namna EU inavyoamiliana na Israel
Sep 14, 2025 07:32Rais wa zamani wa Ireland Mary Robinson amesema, "anaona aibu" kwa mjibizo ambao Umoja wa Ulaya (EU) umeonyesha kwa vita vinavyoendelezwa na Israel huko Ghaza, na akaukosoa umoja huo kwa kushindwa kusimamisha makubaliano yake ya kibiashara na utawala huo wa kizayuni licha ya wito uliotolewa wa kuutaka ufanye hivyo.
-
Bunge la Ulaya lataka kutambuliwa rasmi Palestina Huru
Sep 12, 2025 03:07Bunge la Ulaya limepasisha azimio likielezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya Ukanda wa Gaza, na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuliweka suala la kutambuliwa taifa huru la Palestina kwenye ajenda.
-
Iran yapongeza mazungumzo 'yenye tija' ya Araghchi na Kallas, yaihimiza EU iachane na mtazamo wa makabiliano
Sep 09, 2025 07:36Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema, mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi na Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas ulikuwa wenye tija, na kubainisha kuwa hoja na rai mbalimbali ziliwasilishwa katika mazungumzo yao.
-
"Vikwazo vya Marekani, Ulaya vimeua watu milioni 38 tangu 1970"
Sep 04, 2025 04:12Tahariri iliyoandikwa na tovuti ya habari ya kanali ya televisheni ya al-Jazeera ya Qatar imekosoa muenendo wa nchi za Magharibi kutumia vikwazo kuziadhabu nchi zinazozitazama kama maadui; ikieleza kuwa, vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya vimeua watu zaidi ya milioni 38 kote duniani tangu 1970.
-
Kwa nini zaidi ya wanadiplomasia 200 wa Ulaya wanaukosoa Umoja wa Ulaya kwa kutochukua hatua kuhusu vita vya Gaza?
Aug 29, 2025 06:33Idadi kubwa ya wanadiplomasia wakuu wa zamani wa Ulaya wametaka Umoja wa Ulaya au nchi wanachama wachukue hatua za haraka kuhusiana na vita vya utawala wa Kizayuni huko Gaza na hatua zake zilizo kinyume cha sheria katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Aliyeua watoto kwa bunduki katika skuli ya kanisa Marekani ni mwanamume aliyebadilisha jinsia
Aug 28, 2025 02:36Mshambuliaji aliyefyatulia risasi kanisa katika skuli ya kikatoliki kusini mwa mji wa Minneapolis nchini Marekani jana Jumatano na kuua na kujeruhi watu kadhaa ametambuliwa na gazeti la The New York Post kama Robin Westman. Kwa mujibu wa gazeti hilo, inasemekana Westman alibadilisha jina lake la Robert na kuwa Robin mwaka 2020 na kujitambulisha kama mwanamke.
-
Zaidi ya mabalozi 206 wa zamani wa EU wataka Israel ichukuliwe hatua kali
Aug 26, 2025 22:58Zaidi ya mabalozi 200 wa zamani wa Umoja wa Ulaya na maafisa wa ngazi ya juu jana Jumanne waliituhumu Brussels kwa kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na hali mbaya ya binadamu katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Iran na Ulaya kuendelea na mazungumzo ya nyuklia mjini Geneva
Aug 25, 2025 07:03Iran na nchi tatu zenye nguvu za Ulaya - Ujerumani, Ufaransa na Uingereza - zinatazamiwa kuanza tena mazungumzo ya nyuklia huko Geneva, Uswisi siku ya Jumanne, yakiangazia maswala ya nyuklia na uondoaji wa vikwazo.
-
Iran yaionya Ulaya juu ya matokeo mabaya ya kuamilisha 'snapback'
Aug 23, 2025 02:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ameionya Ulaya juu ya matokeo mabaya ya kuamilisha "utaratibu wa snapback", akisisitiza kwamba Troika ya Ulaya (Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani) pamoja na Umoja wa Ulaya hazina haki ya kisheria na ya kimaadili ya kutumia utaratibu huo.