-
Iraq: Hatuna nia kabisa ya kuwa na uhusiano wa kawaida na Israel
Mar 10, 2021 03:41Ikulu ya Iraq imetoa tamko rasmi la kukanusha madai ya chombo kimoja cha habari cha Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kilichodai kuwa Baghdad iko tayari kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Wazayuni wakizidi kufanya upuuzi tutazisagasaga Tel Aviv na Haifa
Mar 07, 2021 10:16Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, "baadhi ya wakati, na kutokana na kutapatapa, utawala wa Kizayuni hutoa madai makubwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuliko uwezo ulionao ukidhani unaitisha Iran ilhali unajua, na kama haujui, basi ujumbe kwamba ikiwa utazidi kufanya upuuzi tutazisagasaga Tel Aviv na Haifa na kuzisawazisha na ardhi."
-
Kuanza uchunguzi wa ICC wa jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel
Mar 05, 2021 07:04Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, imeanzisha uchunguzi kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.
-
Syria yatuma barua mbili kwa Baraza la Usalama katika kipindi cha masaa 72
Mar 04, 2021 00:43Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetuma barua mbili katika kipindi cha masaa 72 kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulalamikia hujuma dhidi ya mji wa Damascus.
-
Gantz ahofia hatua ya mahakama ya ICC dhidi ya maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel
Mar 03, 2021 10:03Waziri wa vita wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amesema ana wasiwasi juu ya hatua inayoweza kuchukiuliwa na Mahakama ya Kimataifa Jinai ICC dhidi ya maafisa wa utawala huo na akaongeza kuwa, upo uwezekano wa mahakama ya The Hague kuwafuatilia kisheria mamia ya maafisa wa Israel katika faili la jinai za kivita dhidi ya Palestina.
-
Kuongezeka harakati baina ya mhimili wa mapatano wa Kiarabu na utawala haramu wa Israel
Feb 26, 2021 23:15Utata na kutokuwa wazi serikali mpya ya Marekani katika siasa zake za kigeni kuhusiana na eneo la Asia Magharibi ni jambo ambalo limepelea kuongezeka kwa mara nyingine harakati za mhimili wa mapatano wa Kiarabu na utawala haramu wa Israel.
-
Saudia yaongeza kasi ya kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni
Feb 25, 2021 23:21Chombo kimoja cha utawala wa Kizayuni wa Israel kimefichua kuwa viongozi wa Saudi Arabia wameongeza kasi ya kuharakisha kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kwani wanahofia misimamo ya kisiasa ya serikali ya hivi sasa Marekani.
-
HAMAS: Quds ni mji mkuu wa milele wa Palestina
Feb 23, 2021 23:12Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza kuwa, siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuiyahudisha Quds zimeshindwa na kugonga mwamba na kwamba, Quds utabakia kuwa mji mkuu wa milele wa Palestina.
-
Hamas: Kubadilishana mateka, njia pekee ya Israel kuwapata mateka wake
Feb 19, 2021 03:41Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni itawapata wanajeshi wake waliotekwa nyara kupitia tu mpango wa kubadilishana mateka.
-
Video ya Hizbullah iliyokashifu vituo vya kijeshi vya Israel ndani ya miji yazusha taharuki
Feb 18, 2021 22:54Kwa mara ya kwanza, harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa mkanda wa video unaoonyesha kambi na vituo vya kijeshi vya jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndani ya miji ya ardhi hizo za Palestina unazozikalia kwa mabavu.