HAMAS: Quds ni mji mkuu wa milele wa Palestina
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza kuwa, siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuiyahudisha Quds zimeshindwa na kugonga mwamba na kwamba, Quds utabakia kuwa mji mkuu wa milele wa Palestina.
Taarifa iliyotolewa na harakati hiyo ya muqawama ya Palestina imelaani vikali jinai ya hivi karibuni ya Wazayuni ya kubomoa nyumba ya Qadi Aliyan mlinzi wa msikiti wa al-Aqswa na kubakia familia yake bila makazi na kubainisha kuwa, unyama huo wa Israel chimbuko lake nikukasirishwa na hatua ya Mpalestina huyo kuwa mlinzi wa Masjidul-Aqswa.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesema kwa wakazi wa Quds ni askari wa mstari wa mbele katika kukabiliana na njama dhidi ya Msikiti wa al-Aqaswa na miji huo wa mtakatifu kwa ujumla.
Kadhalika Hamas imesema kuwa,utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kushtakiwa kwa mujibu wa sheria za kimataiifa na kuadhibiwa kutokana na jinai zake inazotenda kila uchao dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
Njama hizo za Israel zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongioji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.
Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.
Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyazayunisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.