-
Baqeri: Utawala wa Kizayuni unazidi kudhoofika
Sep 05, 2019 00:04Mkuu wa Kamandi ya Vikosi Vyote vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kambi ya muqawama (mapambano ya Kiislamu) inazidi kusonga mbele katika kuudhoofisha utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo."
-
Ripota wa UN: Matatizo ya ukosefu wa amani Nigeria yapewe mazingatio
Sep 03, 2019 03:37Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa matatizo ya kiusalama ya Nigeria yametengeneza mgogoro ambao unahitajia kupewa mazingatio haraka iwezekanavyo, la sivyo utasababisha ukosefu wa usalama katika nchi nyingine za Kiafrika.
-
Mahakama ya ICC yamtaka Bensouda achunguze tena shambulizi la Israel dhidi ya meli ya Marmara
Sep 03, 2019 03:23Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetaka kufanyike tena uchunguzi kuhusu shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya meli ya Marmara ya Uturuki iliyokuwa na misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Ukanda wa Gaza hapo mwaka 2010.
-
"Israel haina uwezo wa kukabiliana na wanamapambano wa Kiislamu"
Sep 02, 2019 03:12Mtandao maarufu wa habari unaotembelewa na watu wengi nchini Ugiriki umetoa ripoti maalumu na kusema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel hauna uwezo wa kukabiliana na wanamapambano wa Kiislamu wa Hizbullah ya Lebanon.
-
Al Manar: Kamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni aangamizwa kwenye oparesheni ya Hizbullah ya Lebanon
Sep 01, 2019 12:46Televisheni ya al Manar imetangaza kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeangamiza moja ya zana za kijeshi za Israel katika barabara ya al Thakna katika mji wa mpakani wa Israel wa Avivim na kumuua kamanda wa kikosi kimoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika oparesheni iliyotekelezwa na harakati ya Hizbullah.
-
Makampuni ya Imarati yanunua ardhi za mji wa Quds kwa ajili ya Wazayuni
Aug 29, 2019 03:22Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina amesema kuwa makampuni ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) yananunua ardhi huko Quds na kisha kukabidhi umiliki wa ardhi hizo kwa Waisraeli.
-
Al Wifaq: Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain ni muovu zaidi kuliko Wazayuni
Aug 28, 2019 06:31Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al Wifaq) imesema kuwa msimamo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Aal Khalifa wa kutetea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni Israel dhidi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu ni muovu na usio wa kuwajibika.
-
Msemaji wa serikali ya Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel ukubali taathira mbaya za uchokozi wake
Aug 26, 2019 07:31Msemaji wa Serikali ya Iran amelaani mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika nchi za Lebanon, Iraq na Syria na kusema kuwa, utawala huo unapaswa ukubali taathira mbaya za uchokozi huo.
-
Mkuu wa Baraza Kuu la Mashia Lebanon: Israel inachezea moto
Aug 25, 2019 08:01Mkuu wa Baraza Kuu la Mashia nchini Lebanon amesema, kuendeleza utawala wa Kizayuni wa Israel uchokozi dhidi ya Lebanon na Syria ni kuchezea moto, ambao utapelekea kuteketezwa utawala huo.
-
Al Maliki: Iraq itatoa jibu kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Aug 24, 2019 02:28Makamu wa Rais wa Iraq Nouri al Maliki ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Daawa cha Iraq ametoa onyo kali na kusema kuwa, Iraq itatoa jibu kali iwapo itabainika kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umehusika katika shambulizi la angani dhidi ya kituo cha jeshi la kujitolea la wananchi nchini humo maarufu kama Al Hashd al Shaabi.