-
Jeshi la Kizayuni laua shahidi Wapalestina 210 katika 'shambulio la kikatili lisilowahi kushuhudiwa' kwenye kambi ya Nuseirat
Jun 08, 2024 07:50Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imesema, askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya "shambulio la kikatili ambalo halijawahi kushuhudiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat" na kuua kwa umati Wapalestina 210 hadi hivi sasa na makumi ya watu kujeruhiwa mitaani.
-
Sababu za uwezekano wa kutokea vita kati ya utawala wa Kizayuni na Hizbullah ya Lebanon
Jun 08, 2024 01:52Katika hali ambayo utawala wa Kizayuni umeshindwa kufikia malengo yake ya kijeshi uliyoyatangaza katika vita dhidi ya Gaza, vyanzo vya habari vya Kizayuni vimeonya kuhusu harakati za baraza la mawaziri la utawala huo za kutaka kuingia katika vita vya pande zote na Hizbullah ya Lebanon.
-
Jeshi la Kizayuni lakiri kushambulia skuli ya UNRWA Ghaza na kuua Wapalestina 32 wakiwemo watoto
Jun 06, 2024 03:21Jeshi la anga la utawala wa Kizayuni wa Israel alfajiri ya kuamkia leo limeshambulia kwa makombora skuli ya Umoja wa Mataifa katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Ghaza na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 32 wakiwemo watoto na wanawake na kujeruhi makumi ya wengine.
-
Mamia ya Walebanon wameuawa shahidi katika mashambulio ya utawala wa Kizayuni
Jun 06, 2024 03:20Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza kuwa watu 400 wameuawa shahidi tangu jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilipoanzisha mashambulizi dhidi ya nchi hiyo mwezi Oktoba, 2023.
-
Baraza la Wawakilishi la Marekani lakabiliana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC
Jun 06, 2024 01:31Kufuatia ombi la mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) la kutoa kibali cha kukamatwa viongozi wa utawala haramu wa Israel, Baraza la Wawakilishi la Marekani mnamo Jumanne, Juni 4, liliidhinisha mpango wa kuiwekea vikwazo mahakama hiyo ikiwa ni katika kuitetea Tel Aviv kwa hali na mali.
-
Kiwango cha mabomu iliyodondosha Israel Ghaza kimevuka cha Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Jun 05, 2024 03:52Utawala wa Kizayuni wa Israel umedondosha zaidi ya tani 70,000 za mabomu kwenye ardhi ya Ukanda wa Ghaza tangu Oktoba mwaka jana, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi kulinganisha na mabomu yaliyodondoshwa kwenye miji ya Dresden, Hamburg, na London kwa pamoja wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
-
Polisi wa US wakamata waandamanaji 70 baada ya kuvamia ubalozi wa Israel, San Fransisco
Jun 04, 2024 03:47Polisi wa Marekani katika mji wa San Fransisco wamewakamata waandamanaji wapatao 70 wanaotetea na kuunga mkono Palestina baada ya kuingia kwenye ukumbi wa ubalozi mdogo wa utawala wa Kizayuni wa Israel ulioko kwenye mji huo.
-
Adhabu kwa wanachuo wa Marekani wanaounga mkono Palestina
Jun 03, 2024 03:41Makumi ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Chicago nchini Marekani wameondoka katika chuo hicho wakipinga hatua ya bodi ya wakurugenzi ya kukataa kutoa shahada za wanafunzi wanaounga mkono Palestina.
-
Hizbullah ya Lebanon yadungua ndege isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni
Jun 01, 2024 23:40Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imeidungua ndege isiyo na rubani ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya anga ya Lebanon.
-
Bagheri: Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilitokomeza uwezo bandia wa Israel wa kuzuia hujuma
Jun 01, 2024 07:18Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "ubunifu na uamuzi wa Iran wa kumtia adabu mchokozi kwa operesheni ya Ahadi ya Kweli umetokomeza na kufuta uwezo hewa na bandia wa kuzuia hujuma na mashambulio wa utawala wa Kizayuni".