-
Serikali ya Libya kuanzisha operesheni mpya kwa kutumia silaha za Uturuki
May 19, 2019 20:51Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj imetangaza habari ya kupokea zana mpya za kivita, vifaru na magari ya deraya kwa ajili ya kuyatumia katika operesheni zake dhidi ya wapiganaji wa jenerali muasi Khalifa Haftar.
-
Erdogan: Uturuki kuunda na Russia mifumo ya makombora ya S-500
May 19, 2019 08:19Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa nchi yake na Russia kwa pamoja zitaunda mifumo ya makombora ya S-500 baada ya mpango wake wa awali wa kunununua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Moscow kuzusha mivutano.
-
Mchumba wa Khashoggi akosoa kimya cha Marekani kwa mauaji ya mwanahabari huyo wa Saudia
May 17, 2019 02:56Mchumba wa Jamal Khashoggi, mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud aliyeuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki mwaka jana ameitaka Marekani kuanzisha uchunguzi wa mauaji ya kutisha ya mpenzi wake huyo ambaye alikuwa amepanga kufunga naye ndoa kabla ya kuuawa.
-
Uturuki: Tawi la shirika letu la habari Gaza limehujumiwa kwa kufichua maovu ya Israel
May 12, 2019 02:24Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema ofisi ya shirika la habari la nchi hiyo la Anadolu katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu imeshambuliwa na jeshi la utawala haramu wa Israel kwa kufichua 'kazi chafu' na maovu ya utawala huo.
-
Marekani yatishia kuiwekea Uturuki vikwazo vipya ikinunua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Russia
Apr 23, 2019 02:32Uhusiano wa Marekani na Uturuki umekumbwa na msuguano mkubwa hasa baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli ya Julai 2016. Baada ya Uturuki kusambaratisha mapinduzi hayo, ilisema kuwa Marekani ilihusika katika njama hiyo na kwa msingi huo uhusiano wa nchi hizo mbili uliingia baridi.
-
Ahmet Davutoğlu, Waziri Mkuu wa Zamani wa Uturuki amkosoa vikali Rais Recep Tayyip Erdoğan
Apr 22, 2019 22:51Waziri Mkuu wa Zamani wa Uturuki, Ahmet Davutoğlu amemkosoa vikali Rais Recep Tayyip Erdoğan pamoja na siasa za chama tawala cha Uadilifu na Ustawi nchini humo.
-
Sisitizo la Rais Putin la kuweko juhudi za pamoja za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria
Apr 10, 2019 02:09Mgogoro wa Syria na vita vya ndani vya kutwishwa nchi hiyo vilivyoanza 2011, ulipelekea Syria kugeuka na kuwa medani ya makabiliano baina ya Wamagharibi na waitifaki wao wa Kiarabu pamoja na Uturuki hapo awali dhidi ya mhimili wa muqawama ukijumuisha na Russia.
-
Uturuki yakosoa matamshi ya kijuba ya Waziri Mkuu wa Israel
Apr 08, 2019 03:27Uturuki imekosoa vikali matamshi wa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu aliyedai kuwa iwapo ataibuka mshindi katika uchaguzi mkuu ujao, basi atauunganisha rasmi Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na maeneo mengine ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu, chini ya mpango wa Marekani wa "Muamala wa Karne".
-
Kutimuliwa NATO, tishio lisilo na kifani la Marekani dhidi ya Uturuki
Apr 04, 2019 10:17Uhusiano wa Marekani na Uturuki umekuwa mbaya katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita hasa baada ya jaribio la kuipindua serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan manamo Junia 15 mwaka 2016.
-
Ankara: Marekani ichague ama kushirikiana na Uturuki au magaidi
Apr 04, 2019 03:23Makamu wa Rais wa Uturuki amejibu matamshi ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, ambaye aliitaka Ankara inunue ndege za kivita za F-35 kutoka Marekani badala ya kununua mfumo wa kujilinda na mashambulizi ya makombora wa S-400 kutoka kwa Russia.