-
Uturuki kuujenga upya mji 'wake' wa kale wa bandari huko Sudan
Dec 27, 2017 12:17Sudan imesema kuwa Uturuki itaujenga upya mji wa bandari ulioharibiwa wakati wa zama za Othmaniya unaopatikana katika Ukanda wa pwani ya Sudan huko katika Bahari Nyekundu, ikiwa ni katika juhudi za Ankara za kupanua mahusiano yake ya kijeshi na kiuchumi barani Afrika.
-
Uturuki na Sudan zakubaliana kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili
Dec 25, 2017 11:26Uturuki na Sudan zimekubaliana kuanzisha baraza la ushirikiano wa kistratejia na kuzidisha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi mbili hizo kufuatia ziara ya kihistoria iliyofanywa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Khartoum.
-
Baada ya kushindwa njama zao dhidi ya Qatar na Yemen, kundi la Saudia lamalizia hasira zake kwa Uturuki
Dec 20, 2017 12:54Serikali ya Uturuki imekasirishwa sana na hatua ya waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) aliyetuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtuhumu Rais Recep Tayyip Erdogan kuwa ni kutoka kizazi cha Waturuki waliofanya wizi mjini Madina na kukandamiza Waarabu wakati wa utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire).
-
Uturuki: Baadhi ya nchi za Kiarabu zinaiogopa mno Marekani
Dec 13, 2017 00:23Uturuki imekosoa kile ilichokieleza kama hatua na msimamo dhaifu wa nchi za Kiarabu kuhusiana na uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuitambua Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais Rouhani kushiriki mkutano wa dharura wa OIC, Quds ndiyo ajenda kuu
Dec 12, 2017 04:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo anaelekea Uturuki kwa shabaha ya kushiriki katika kikao cha dharura cha viongozi wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) nchini Uturuki.
-
Lawama kali za Erdogan kwa uingiliaji wa Marekani; asema Marekani ndiyo iliyoiunda na kuipa silaha ISIS
Nov 20, 2017 02:34Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amelalamikia vikali uingiliaji wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na kuahidi kuwaangamiza magaidi wote wanaotumia eneo la kaskazini mwa Iraq kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya nchi yake.
-
Rais Erdoğan aichoma moyo Saudia, asisitiza kuendelea kuiunga mkono Qatar
Nov 16, 2017 04:39Katika kile kinachonekana kuwa ni kuwachoma moyo viongozi wa Saudi Arabia katika mgogogro unaoendelea kati ya nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesisitizia uungaji mkono wake kwa Qatar.
-
Rais wa Uturuki akosoa kauli ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi kuhusu Uislamu
Nov 12, 2017 04:08Katika msururu wa kurushiana maneneo viongozi wa Saudi Arabia na Uturuki, Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki amekosoa vikali matamshi ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia Mohammad Bin Salman kuhusu kile alichodai kuwa ni "Uislamu wa misimamo ya wastani."
-
Ombi la Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq kwa Iran na Uturuki
Oct 08, 2017 09:51Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq kupitia taarifa rasmi iliyoiwasilisha kwa balozi za Iran na Uturuki mjini Baghdad, imezitaka nchi hizo mbili sambamba na kufunga vivuko vyote vya eneo la Kurdistan ya Iraq, kusimamisha pia miamala ya mauziano ya mafuta na eneo hilo.
-
Mkakati wa Uturuki wa kutaka kustawisha ushirikiano wa kiulinzi na kiusalama na Iraq
Oct 07, 2017 03:14Waziri Mkuu wa Uturuki amesema, kufuatia kura ya maoni iliyofanyika hivi karibuni katika eneo la Kurdistan ya Iraq, nchi yake inataka kuimarisha ushirikiano na serikali kuu ya Iraq katika nyuga za uchumi, ulinzi na usalama.