Uturuki na Sudan zakubaliana kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38099-uturuki_na_sudan_zakubaliana_kuimarisha_uhusiano_kati_ya_pande_mbili
Uturuki na Sudan zimekubaliana kuanzisha baraza la ushirikiano wa kistratejia na kuzidisha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi mbili hizo kufuatia ziara ya kihistoria iliyofanywa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Khartoum.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2017 11:26 UTC
  • Uturuki na Sudan zakubaliana kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili

Uturuki na Sudan zimekubaliana kuanzisha baraza la ushirikiano wa kistratejia na kuzidisha mahusiano ya kibiashara kati ya nchi mbili hizo kufuatia ziara ya kihistoria iliyofanywa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Khartoum.

Erdogan jana aliwasili Khartoum mji mkuu wa Sudan ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu itakayompeleka pia katika nchi za Chad na Tunisia. Akiwa katika mazungumzo na mwenzake wa Sudan Omar Hassan al Bashir huko Khartoum, Rais wa Uturuki amesema kuwa  nchi mbili hizo zimeazimia kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara kutoka kiwango cha sasa cha dola milioni 500 kwa mwaka na kufikia dola bilioni moja kwa kuanzia na baadaye kiwango hicho kuboreshwa zaidi na kufika dola bilioni kumi kwa mwaka.

Marais wa Uturuki na Sudan wakiwa mjini Khartoum 

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amewatolea wito wafanyabiashara kuwekeza nchini Sudan na kuongeza kuwa nchi yake inafahamu vyema kuhusu nguvu ya kiuchumi ya Sudan. Hii ni ziara ya kanza kuwahi kufanywa huko Sudan na Rais wa Uturuki tangu Sudan ipate uhuru mwaka 1956.  Kwa upande wake Rais al Bashir wa Sudan amesema kuwa ziara ya Rais Erdogan itaimarisha uhusiano kati ya nchi mbili hizo za Kiislamu. Marais wa Sudan na Uturuki wamejadili pia hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuutambua rasmi mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.