Rais Erdoğan azionya Marekani na Israel kuhusiana na kadhia ya Quds
https://parstoday.ir/sw/news/world-i38319-rais_erdoğan_azionya_marekani_na_israel_kuhusiana_na_kadhia_ya_quds
Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amezionya serikali ya Marekani na utawala wa Kizayuni juu ya hatua zao za kuchukua maamuzi dhidi ya mji wa Quds (Jerusalem).
(last modified 2026-05-10T14:24:40+00:00 )
Dec 31, 2017 00:01 UTC
  • Rais Erdoğan azionya Marekani na Israel kuhusiana na kadhia ya Quds

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amezionya serikali ya Marekani na utawala wa Kizayuni juu ya hatua zao za kuchukua maamuzi dhidi ya mji wa Quds (Jerusalem).

Erdoğan ametoa indhari hiyo kupitia ujumbe alioutuma kwenda kongamano la 16 la Waislamu ambalo ni la kila mwaka lililofanyika mjini Chicago, Marekani ambapo pia amepongeza uungaji mkono wa ulimwengu wa Kiislamu kwa kadhia ya Quds. Aidha katika ujumbe huo kwa kongamano hilo lililoitishwa na Jumuiya ya Waislamu wa Marekani (MAS) na Muungano wa Kiislamu wa Amerika ya Kaskazini (ICNA), Rais Erdoğan wa Uturuki ameongeza kuwa hatua ya nchi 128 kupinga katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) tangazo la Trump la kuutambua mji wa Quds kuwa mji mkuu wa Israel, inatakiwa iache alama ya swali kwa viongozi wa Marekani sambamba na  kubadili mienendo yao kuhusiana na mji wa Quds.

Msikiti wa Quds ambao unakabiliwa na njama chafu za Marekani na Israel

Kongamano la kila mwaka la 16 kwa ajili ya Waislamu (MAS) Muungano wa Kiislamu wa Amerika ya Kaskazini (ICNA), lilihudhuriwa na watu wengi mjini Chicago ambapo kuliwasilishwa maudhui mbalimbali zinazowahusu Waislamu duniani likiwemo pia suala la ongezeko la chuki na ubaguzi dhidi ya Waislamu hao ndani ya madola ya Magharibi. Mbali na Erdoğan mataifa mbalimbali ya Kiislamu ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimesimama imara kuitetea Quds sambamba na kukabiliana na njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.