-
Pakistan: Tunafanya juhudi za kuzirudisha Marekani na Iran kwenye meza ya mazungumzo
Sep 12, 2026 04:23Balozi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amesema: "tunafanya juhudi za kuzirudisha Marekani na Iran kwenye meza ya mazungumzo".
-
Jenerali Mohsen Rezaei: Marekani impokea ‘onyo la wazi’ kutoka kwa makombora mapya ya Iran
Sep 08, 2026 11:24Afisa mkuu wa usalama wa Iran amesema kuwa Marekani imepokea “onyo la wazi” kutokana na uwezo mpya wa makombora wa Jamhuri ya Kiislamu, baada ya Tehran kufanya majaribio ya kombora jipya la kupambana na meli za kivita karibu na meli ya kivita ya Marekani katika maji ya kikanda.
-
Makombora ya Balistiki ya IRGC yalazimisha meli za Kivita za Marekani kutoroka
Sep 06, 2026 04:20Kikosi cha Anga za Juu cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimerusha makombora kadhaa ya balistiki kuelekea kwenye manowari mbili za Marekani ikiwemo ile yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita na kuzilazimu kutoroka. Meli hizo za kivita zilikuwa zikishiriki katika mzingiro haramu wa baharini wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran: Baraza la Usalama la UN lilaani shambulio la Marekani lililoua raia kwenye sherehe ya harusi
Sep 03, 2026 03:19Iran imeliitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani shambulio la Marekani lililolenga nyumba ya makazi iliyokuwa ikiandaa sherehe ya harusi kusini mwa Jamhuri ya Kiislamu, ambalo limesababisha kuuawa shahidi wa raia watano, akiwemo mtoto wa miaka minne, na kuwajeruhi zaidi ya watu 70 wengine.
-
Waziri wa Fedha wa Ujerumani amwambia Trump: Komesha vita 'visivyo na uwajibikaji' dhidi ya Iran
Aug 29, 2026 10:14Waziri wa Fedha wa Ujerumani amemtaka Rais Donald Trump wa Marekani kukomesha vita "visivyo vya kuwajibika" dhidi ya Iran.
-
Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran: Iran kupanua kwa mafanikio mifumo ya ulinzi
Aug 27, 2026 04:24Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran amesema kuwa Iran inapiga hatua mbele kwa kutegemea kikamilifu uwezo wake wa ndani, ikipanua mifumo yake ya ulinzi wa anga na kuzalisha nakala za mifumo ile iliyofanya vyema wakati wa vita vya siku 40.
-
Malik Agar: Chaguo letu ni suluhisho la kijeshi hadi mazingira ya mazungumzo yatakapotimizwa
Aug 23, 2026 14:19Malik Agar, naibu mkuu wa Baraza Kuu la Utawala nchini Sudan, amesema kwamba chaguo la sasa ni suluhisho la kijeshi mpaka pale mazingira ya kufanyika mazungumzo yatakapotimizwa, akisisitiza kwamba Khartoum inalitaka kundi la Rapid Support Forces (RSF) kuondoka katika miji na maeneo ya makazi ya raia kabla ya mazungumzo yoyote kuanza.
-
Iran yamtahadharisha Trump kuhusu 'fikra potofu' ya kudai Mlango-Bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani
Aug 19, 2026 04:16Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa Marekani kwa madai yake kuhusu Lango la Bahari la Hormuz, akionya kuwa "fikra yake potofu" ya kuihesabu njia hiyo muhimu ya maji kama "eneo jipya la Marekani" inapasa kurekebishwa, la sivyo Tehran itamweka sawa.
-
Mtawala wa Dubai 'azongwa' kwenye mitaa ya London kwa kuhusika UAE katika vita vya Sudan
Aug 12, 2026 03:31Mtawala wa Dubai ambaye ni waziri mkuu wa Muungano wa Falme za Kiarabu, UAE amezongwa kwa maneno katika mitaa ya katikati mwa mji mkuu wa Uingereza, London kuhusiana na ushiriki wa nchi yake katika vita vya ndani nchini Sudan.
-
Yemen yavishambulia vituo vya nishati vya Saudi baada ya nchi hiyo kukiuka anga ya Sa’adah na Hajjah
Aug 09, 2026 11:00Yemen imeishambulia miundombinu ya nishati ya Saudi Arabia ikiwa ni jibu kwa ndege zisizo na rubani za adui zinazokiuka anga ya mikoa ya Sa’adah na Hajjah huko Yemen.