-
"Save Sudan"... Kampeni kuu kwenye mitandao ya kijamii ikiangazia yanayojiri nchini humo
Dec 22, 2023 03:06Wanaharakati wa mitandao ya kijamii wameanzisha kampeni kubwa iliyopewa jina la Save Sudan inayoangazia na kumulika masaibu yanayowapata wananchi wa Sudan kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo na kupuuzwa na jamii ya kimataifa hasa vyombo vya habari ambavyo aghlabu vimeelekeza mazingatio yao huko Gaza na mauaji ya raia wa Palesrina yanayofanywa na Israel.
-
Madhara ya kuendelea vita baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan
Sep 23, 2023 06:24Licha ya kupita miezi mingi, lakini ndio kwanza vita baina ya majenerali wa kijeshi vinaendelea nchini Sudan na hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hiyo inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku. Cha kusikitisha ni kuwa pamoja na hali kuwa mbaya kiasi hicho, lakini bado pande hasimu zinaendelea kufanya ukaidi wa kutokubali kusimamisha mapigano.
-
Al Burhan atembelea Juba huku vita vikiendelea nchini Sudan
Sep 04, 2023 12:57Rais wa Baraza la Utawala wa Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, mapema leo alikuwa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, kwa ziara rasmi ya siku moja, kujadili hali ya Sudan na uhusiano kati ya nchi hizo mbili, huku mapigano makali yakiendelea kuripotiwa nchini kwake.
-
Al Burhan akutana na al Sisi mjini Cairo katika safari ya kwanza nje ya nchi baada ya kuanza vita Sudan
Aug 29, 2023 11:51Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, leo Jumanne amewasili nchini Misri, katika ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu kuanza mapigano ya ndani nchini Sudan yapata miezi 5 iliyopita, huku mapigano yakiendelea kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa Khartoum na maeneo mengine.
-
Taharuki yatanda nchini Niger baada ya ECOWAS kuamua tarehe ya kuishambulia nchi hiyo
Aug 20, 2023 02:28Mji mkuu wa Niger, Niamey, unashuhudia vuguvugu na taharuki kubwa ya jeshi na wananchi wanaowaunga mkono viongozi wa mapinduzi wakipinga uwezekano wa uingiliaji kijeshi wa nchi wanachama wa Jumuiya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) nchini humo.
-
Jarida la Wall Street: Imarati imetuma silaha kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko Sudan
Aug 11, 2023 07:56Jarida la Kimarekani la Wall Street Journal limefichua katika ripoti yake kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu unatoa misaada ya kijeshi kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), vinavyopigana na jeshi la Sudan kwa miezi kadhaa sasa.
-
Amnesty International: Uhalifu wa kutisha wa kivita unafanyika nchini Sudan
Aug 04, 2023 12:09Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema katika ripoti yake mpya kwamba uhalifu mkubwa wa kivita unafanywa nchini Sudan, na kwamba raia kote nchini humo wanaishi katika hufo na woga "usiofikirika".
-
Indhari ya Katibu Mkuu wa UN ya kufikia Sudan kwenye ukingo wa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe
Jul 11, 2023 11:30Mapigano nchini Sudan yanaendelea kupamba moto, na juhudi zilizofanywa hadi sasa za kuleta suluhu na kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo sio tu hazijafanikiwa, lakini pande mbili zinazopigana zimeshadidisha pia mashambulizi yao. Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha kuwa, Sudan sasa imeshafika kwenye ukingo wa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.
-
Wafadhili waahidi kutoa msaada wa dola bilioni 1.5 kwa ajili ya Sudan
Jun 20, 2023 08:05Wafadhili wameahidi katika Mkutano wa Geneva wa Kukabiliana na Mgogoro wa Sudan, kutoa msaada wa kibinadamu wa takriban dola bilioni 1.5, wakati huu ambapo hali ya utulivu imetanda kwa kiasi fulani nchini Sudan kwa siku ya pili kutokana na makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa baina ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
UN yalaani ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita Sudan, mapigano makali yaripotiwa Khartoum
May 19, 2023 10:31Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu, Martin Griffiths, amelaani kile alichokitaja kuwa ukiukwaji wa mara kwa mara na mkubwa wa makubaliano yaliyofikiwa wiki moja baina ya pande zihasimu katika mzozo wa Sudan ya kulinda maisha ya raia, harakati za misaada ya kibinadamu na miundombinu.