-
Maafa ya vifo vya wakimbizi katika mfereji wa Manch, matokeo ya mzozo kati ya Ufaransa na Uingereza
Nov 27, 2021 11:28Zaidi ya wakimbizi 27 kutoka pwani ya kaskazini ya Ufaransa waliovuka Mfereji wa Manchi wakijaribu kufika katika ardhi ya Uingereza walighariki na kufariki Jumatano jioni, Novemba 24, baada ya boti yao kuzama.
-
Maafa ya wahajiri kuelekea Ulaya; watu zaidi ya 75 wazama katika pwani ya Libya
Nov 21, 2021 04:48Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kuwa, wahamiaji haramu zaidi ya 75 wamefariki dunia baada ya boti yao kuzama katika pwani ya magharibi mwa Libya. Wahajiri hao haramu wamekumbwa na mauti Jumatano iliyopita katika jitihada za kuelekea barani Ulaya.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa vitendo vya mabavu vya nchi za Ulaya dhidi ya wakimbizi
Nov 13, 2021 08:19Akizungumza katika bunge la Ulaya Filippo Grandi Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amekosoa vitendo vya mabavu na ukandamizaji wa Umoja wa Ulaya dhidi ya wakimbizi na kusisitiza kuwa siku zote na mara kwa mara tunashuhudia raia wanaotafuta hifadhi barani Ulaya wakifukuzwa kwa mabavu na visingizio vya kisheria kutumika katika kuwanyima hifadhi raia hao.
-
Kupamba moto mgogoro wa wakimbizi barani Ulaya
Nov 11, 2021 07:10Kwa mara nyingine tena, wimbi la wakimbizi wanaomiminika kwenye mipaka ya nchi za Ulaya limeongezeka na kuwa mgogoro mkubwa. Nchi za Ulaya zimeamua kufunga mipaka yao ili kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wapya.
-
Maelfu ya wakimbizi wa Kiafghani wanaingia Iran kila siku
Nov 11, 2021 04:39Shirika moja la Ulaya la kushughulikia maslahi ya wakimbizi limeiasa jamii ya kimataifa kuwapa msaada wa chakula na makazi maelfu ya wakimbizi wanaoingia nchini Iran kila siku wakitokea Afghanistan.
-
Syria: Mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi ni haki ya nyakati zote
Sep 24, 2021 03:08Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Syria amesema kuwa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi ni haki isiyomalizika na ya nyakati zote.
-
Wakimbizi kutoka Afghanistan waanza kuwasili Uganda
Aug 25, 2021 08:27Kundi la kwanza la makumi ya wakimbizi kutoka Afghanistan limewasili nchini Uganda.
-
Mgogoro wa wakimbizi; italia yataka kuitishwe kikao maalumu cha kutafuta suluhisho
Aug 05, 2021 21:54Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia ametoa wito wa kuitishwa kikao maalumu cha kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa wakimbizi na kugawana wakimbizi hao baina ya nchi za Ulaya kwa uadilifu.
-
Mamia ya wakimbizi wa Kongo DR wamiminika Uganda
Jun 16, 2021 21:59Wakimbizi karibu elfu moja raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewasili nchini Uganda katika kipindi cha siku chache zilizopita.
-
UN yaingilia kati mpango wa Kenya wa kufunga kambi kuu za wakimbizi
Apr 10, 2021 03:42Shirika la Kuhudumua Wambizi la Umoja wa Mataifa UNCHR kupitia taarifa iliyotolewa jana mjini Geneva Uswisi, limetangaza kushirikiana na Kenya na kuweka mapendekezo ya hatua za kuchukua ili kupata suluhisho kwa mgogoro wa wakimbizi wanaoishi katika kambi za Dadaab na Kakuma za nchi hiyo ya Afrika Mashariki.