-
Kuongezeka kukosolewa uungaji mkono wa Magharibi kwa utawala wa Kizayuni
Nov 16, 2023 04:11Kuendelea jinai , mauaji ya kimbari na kutokomezwa kizazi cha wananchi wa Gaza na utawala wa Kizayuni ambazo zimesababisha maelfu ya Wapalestina kuuawa shahidi na kujeruhiwa, kumepelekea kushtadi kukosolewa siasa za upendeleo za serikali za Magharibi kwa Israel.
-
Kuongezeka hasira za kimataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza
Nov 12, 2023 03:07Sambamba na kuendelea vitendo vya jinai vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, ambavyo hadi sasa vimepelekea kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina elfu 11 na kujeruhiwa wengine zaidi ya elfu 27, hasira na ukosoaji wa kimataifa unaendelea kuongezeka kwa kadiri kwamba mbali na maandamano makubwa yanayofanyika katika pambe tofauti za dunia, baadhi ya wanasiasa wa Magharib pia wanaukosoa utawala huo kutokana na ukatili wake wa kutisha dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
-
Marekani na kukana mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza
Nov 08, 2023 02:41Zaidi ya mwezi mmoja umepita sasa tangu kuanza kwa vita vya Gaza na tangu kutekelezwa kwa operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" huku utawala wa Kizayuni unaoendesha operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza dhidi ya wapiganaji wa Hamas ukizidisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya eneo hilo. Mashambulio hayo ya kinyama ya Israe; yameendelea kusababisha mauaji makubwa ya watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza.
-
Kuongezeka upinzani dhidi ya vitendo vya kijinai vya utawala wa Kizayuni katika nchi za Magharibi
Nov 07, 2023 02:31Mwezi mmoja ukiwa umepita tangu kujiri operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na utawala wa Kizayuni kuanzisha mashambulizi makali ya mabomu ambayo hajawahi kushuhudiwa tena huko Ghaza, ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya maelfu ya Wapalestina, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, mwenendo wa upinzani dhidi ya vitendo hivyo vya jinai vya Israeli, umeongezeka sana duniani ikiwa ni pamoja na nchini Marekani, ambayo ni mwitifaki mkubwa wa Tel Aviv.
-
Kupasishwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ghaza
Oct 28, 2023 12:09Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha rasimu ya azimio lililopendekezwa na nchi za Kiarabu na kutaka kutekelezwa usitishaji vita wa kibinadamu haraka iwezekanavyo huko Ghaza.
-
Kupigiwa kura ya veto maazimio yanayohusu vita vya Ghaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Oct 27, 2023 07:27Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limeshindwa kupasisha azimio Katika hali ambayo wananchi wa Ukanda wa Ghaza bado wanakabiliwa na mashambulizi ya kinyama na ya kutisha ya utawala wa Kizayuni ambapo utawala huo unazuia kufikishwa misaada ya dharura katika eneo hilo.
-
Upinzani mkali wa Marekani dhidi ya juhudi za kusitisha vita Ghaza
Oct 24, 2023 10:03Marekani ikiwa ni mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni si tu kwamba inatoa misaada ya kila aina ya silaha na fedha kwa ajili ya kuushambuliwa Ukanda wa Ghaza, bali pia inapinga vikali usitishwaji vita katika uvamizi huo wa umwagaji damu kwa visingizio vya uongo na visivyo na msingi.
-
Vipimo viwili tofauti vya Ulaya kuhusu uhuru wa kujieleza; vitisho na adhabu kwa waungaji mkono wa Palestina
Oct 22, 2023 02:37Matukio ya hivi karibuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel hasa baada ya mashambulizi ya Kimbunga cha Al-Aqsa na jibu la kinyama la utawala wa Kizayuni, hasa mashambulizi ya kikatili ya utawala huo dhidi ya wanawake na watoto wa Ukanda wa Ghaza, yameibua radiamali kali ya jamii ya kimataifa dhidi ya utawala huo.
-
Kikao kisichokuwa na natija cha Baraza la Usalama: Marekani yapinga usitishaji mapigano Gaza
Oct 19, 2023 10:50Jumatano, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikataa tena azimio la kusitisha mapigano huko Gaza kufuatia upinzani wa Marekani. Marekani ilipinga azimio lililopendekezwa kwa Baraza la Usalama na Brazil, lililotaka kusitishwa mapigano ili kufikishwa misaada ya kibinadamu Ghaza.
-
Jitihada za Magharibi za kuzuia kuakisiwa habari za Wapalestina katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari
Oct 15, 2023 02:23Baada ya kuanza oparesheni kwa jina la "Kimbunga cha Al Aqsa" iliyotekelezwa na Hamas na makundi mengine ya mapambano ya Palestina; serikali na vyombo vya habari vya Magharibi kwa upande mmoja vimeanzisha propaganda kubwa ili kuzuia kuakisiwa habari na matukio yanayojiri huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu huku vikichapisha na kutoa habari za uwongo ili kuonyesha taswira isiyo ya kibinadamu kuhusu wanamapambano wa Palestina.