Kupasishwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ghaza
(last modified Sat, 28 Oct 2023 12:09:26 GMT )
Oct 28, 2023 12:09 UTC
  • Kupasishwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ghaza

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha rasimu ya azimio lililopendekezwa na nchi za Kiarabu na kutaka kutekelezwa usitishaji vita wa kibinadamu haraka iwezekanavyo huko Ghaza.

 Azimio hilo lilipasishwa jana usiku kwa kura 120 za ndio mkabala wa 14 za hapana huku nchi 45 zikijizuia kupiga kura. Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani zimelipigia azimio hilo kura ya hapana. 

Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tokea kuanza mapigano kati ya makundi ya mapambano ya ukombozi wa Palestina na utawala wa Kizayuni hadi sasa zilikuwa zimeshindwa kupasisha azimio lolote kwa ajili usitishaji vita wa haraka huko Ghaza. 

Nukta ya kufurahisha ni kuwa, jitihada za nchi za Magharibi za kutaka kujumuisha baadhi ya vifungu katika azimio hilo vinavyolaani mapambano ya wananchi wa Palestina dhidi ya adui ghasibu zimegonga mwamba. Kuhusiana na suala hilo, hatua ya Canada ya kutaka kupatikana uungaji mkono kwa Israel na kukwamisha azimio hilo lililopendekezwa na nchi za Kiarabu, imeambulia patupu. Canada, ikiungwa mkono na Marekani, iliwasilisha marekebisho kwa jaili ya azimio hilo na ilitaka kulaaniwa kile illichokitaja kuwa "mashambulizi ya kigaidi ya Hamas" dhidi ya utawala ghasibu wa Israel. 

Wanamuqawama wa Palestina 

Kupasishwa azimio hilo na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika hatua yake ya kwanza kwa ajili ya kutekeleza haraka iwezekanavyo usitishaji vita huko Ghaza kunaonyesha kuwajibika na takwa la jamii ya kimatiafa la kuhitimisha jinai na hatua zilizo dhidi ya binadamu za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina haraka iwezekanavyo hususan wakazi wa Ukanda wa Ghaza ambao kwa zaidi ya wiki tatu sasa wanakabiliwa na mashambulizi makubwa ya mabomu ya Israel. Mashambulizi hayo hadi sasa yameuwa shahidi zaidi ya watu elfu 7, kujeruhi karibu elfu 20 na kuharibu sehemu kubwa ya Ukanda wa Ghaza.

Vassily Nebenzia Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa kupasishwa azimo na Baraza Kuu la UN kuhusu Ghaza kunadhihirisha ushindi wa akili ya kawaida na haki. Nebenzia amesema: Azimio hilo ni ushindi wa akili yenye afya, haki na mazingingatio ya ubinadamu. 

Vassily Nebenzia 

Wakati huo huo, kupasishwa azimio hilo na Baraza Kuu la UN kuhusu Ghaza kuna maana ya aina fulani ya kujitoa kwenye mkwamo wa sasa ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu upasishaji wa azimio la kusitisha vita huko Ghaza. Baraza la Usalama, kutokana na muundo wake maalumu na pia mamlaka ya udhibiti ya nchi tano wanachama wa kudumu, yaani nchi zenye haki ya kura ya turufu (veto), hadi sasa limeshindwa kufikia muafaka kwa sauti moja ili kupasisha azimio kla kuhitimisha vita vya Ghaza kutokana na mitazamo kinzani ya  nchi wanachama wa kudumu wa kambi ya Magharibi yaani Marekani, Uingereza na Ufaransa kwa upande mmoja, na kambi ya Mashariki yaani Russia na China kwa upande wa pili. 

Wakati huo huo hatua ya wanachama wa kambi ya Magharibi katika Baraza la Usalama la UN wakiongozwa na Marekani ya kushinikiza kutotekelezwa usitishaji vita huko Ghaza; na katika upande mwingine, kushutumiwa makundi ya muqawama ya Palesetina hasa harakati ya Hamas kumekabiliwa na upinzani wa Russia na China zilizopinga rasimu ya azimo lililowasilishwa na Marekani. Katika upande mwingine, Washington pia imepinga vifunguu vya maazimio yaliyopendekezwa na Russia baada ya kutokubaliana na vifungu vyake kikiwemo kifungu kinachosisitiza ulazima wa kusitishwa vita mara moja huko Ghaza. Kwa hakika Marekani ikiwa ndio muungaji mkono mkuu na wa bila masharti yoyote wa utawala wa Kizayuni, haitaki kuona Israel ikikabiliwa na vikwazo na mshinikizo kwa hatua zake dhidi ya Wapalestina na makundi ya muqawama.

Katika uwanja huo, White House leo asubuhi imetangaza kuwa haijalitwisha lolote jeshi la utawala wa Kizayuni wala kuliainishia mstari mwekundu. John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama la Ikulu ya Rais wa Marekani, White House amesema: Hatujaiainishia Israel  mstari wowote mwekundu. Tunaendelea kuipatia Israel misaada ya kiusalama inayohitajia." Marekani inahalalisha jinai za utawalal wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Ghaza katika hali ambayo inazitaja hatua za Hamas za kukabiliana na maghasibu wa Kizayuni kuwa vitendo vya kigaidi. katika muktadha huo Joe Biden amekiri kwamba raia wengi wa Kipalestina wamepoteza na akasema: Idadi hiyo ya vifo ni sehemu ya gharama za vita. Jambo hili kwa mara nyingine tena limedhihirisha misimamo ya kinafiki na undumakuwili ya Marekani. Hivi sasa utawala wa Kizayuni unaendeleza mauaji ya kikatili dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza kwa kupewa ruhusa na kuungwa mkono kisiasa na kijeshi wa Marekani,  huku Washington ikipinga na kuzuia azimio lolote dhidi ya jinai za utawala haramu wa Kizayuni.

Tags