Jeffrey Sachs: Marekani, Israel na Uturuki wanahusika na machafuko ya Syria
Pars Today - Mchambuzi wa Marekani amesema kuwa, machafuko nchini Syria ni sehemu ya mpango wa pamoja wa Marekani, Israel na Uturuki.
Sambamba na kutekwa kwa Damascus na vikundi vyenye silaha, mahojiano ya hivi karibuni ya Profesa "Jeffrey Sachs" na "Pierce Morgan" kwenye mtandao wa kijamii wa X yalitembelewa kwa wingi. Kulingana na Pars Today, Profesa "Jeffrey Sachs" alisema katika mahojiano na "Piers Morgan" mnamo Desemba 6, ambapo aliashiria machafuko nchini Syria na kusema:
"Hii ni operesheni ya Marekani, Israel na Utuuruki. Hii ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye amekuwa akifanya kazi kwa miaka 30 kupindua serikali zinazounga mkono kadhia ya Palestina katika eneo lote la Mashariki ya Kati.