Ni kitu gani vyombo vya habari vya Magharibi vinakiita "uhuru"?
Parstoday- Mtumiaji wa Iran wa mtandao wa kijamii wa X ameashiria nafasi na mchango wa vyombo vya habari vya magharibi katika matukio ya Syria katika ujumbe wake na kukosoa utendaji wao wa kindumakuwili kuhusiana na mafuhumu na maana ya uhuru.
Elham Abedini, mtumiaji wa Kiirani wa mtandao wa kijamii wa X, almechapisha picha ya moto na moshi unaoteketeza Damascus, Syria, na kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: Hii ni Damascus na Israel inashambulia kwa mabomu mji mkuu wa Syria. Kulingana na Parstoday, Abedini ameongeza: Mashambulizi haya ni katika wakati ambapo utawala wa Kizayuni unaendelea kushambulia vijiji vya kusini mwa Lebanon licha ya kile kinachoitwa "kusitisha mapigano" na umekuwa ukiilenga Gaza bila kuchoka.
Abedini anafafanua zaidi: Hiki ndio kile kitu ambacho vyombo vya habari vya magharibi vinakiita “uhuru”!
Ikumbukwe kuwa kufuatia matukio ya Syria na kutekwa Damascus na magaidi na wapinzani wenye silaha, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumapili alitangaza kusambaratika makubaliano ya "kutengana" kati ya Syria na utawala wa Kizayuni mwaka 1974 katika eneo la Golan na aliamuru eneo Golan inayokaliwa kwa mabavu kuwa litakuwa chini ya udhibiti wa utawala huo ghasibu.
Kufuatia hatua hiyo, vyanzo vya habari vilitangaza kukaliwa kwa mabavu maeneo ya ardhi ya Syria na jeshi la Kizayuni na kuchapisha picha za kujipenyeza kwa majeshi ya utawala ghasibu wa Kizayuni katika mkoa wa Quneitra nchini Syria. Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Wazayuni walipenya umbali wa kilomita 14 ndani ya ardhi ya Syria.