Iran ina silaha ambazo adui hana taarifa nazo kabisa
(last modified Mon, 13 Jan 2025 06:57:35 GMT )
Jan 13, 2025 06:57 UTC
  • Iran ina silaha ambazo adui hana taarifa nazo kabisa

Kamanda mmoja wa ngazi za juu wa Jeshi la Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina silaha ambazo hazijafichuliwa hadi sasa na wala adui hana taarifa zozote kuhusu silaha hizo.

Press TV imetuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X ikimnukuu, Naibu Mkuu wa Majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani aliyasema hayo jana Jumapili alipokuwa akizungumzia mazoezi ya kijeshi ya  Jeshi la Iran kwa ajili ya kuonesha ustadi na utayari wake wa kukabiliana na vitisho vya adui. 

Jenerali Ashtiani ametamka hayo mbele ya waandishi wa habari na kusisitiza kwa kusema: “Tuna silaha ambazo hatujawahi kuzizungumzia hadi sasa na adui hana taarifa zozote kuhusu silaha hizo. Baadhi ya silaha hizo zinaweza kujaribiwa wakati wa mazoezi  ya kijeshi.”