Watalii kadhaa wa utawala wa Kizayuni wauawa Misri
(last modified Sun, 08 Oct 2023 12:53:57 GMT )
Oct 08, 2023 12:53 UTC
  • Watalii kadhaa wa utawala wa Kizayuni wauawa Misri

Watalii kadhaa wa utawala wa Kizayuni wameuliwa kwa kupigwa risasi huko Misri. Kwa mujibu wa Al Jazeera, duru moja ya usalama ya Misri imetangaza kuwa askari polisi wa nchi hiyo amewauwa kwa kuwapiga risasi watalii wawili wa Israel nchini humo. Polisi huyo wa Misri alitumia silaha yake binafsi kutekeleza mauaji hayo

Wakati huo huo, baadhi ya vyanzo vingine vya habari, katika ripoti zinazokinzana, vilitangaza idadi ya watu waliouawa kwa kupigwa risasi nchini Misri kuwa ni watu 7, huku wengine wakitangaza kuwa 6 wamefariki na 8 kujeruhiwa.

Kanali ya 14 ya utawala wa Kizayuni imeripoti kuwa, basi lililokuwa limebeba watalii wa Kizayuni lilipigwa risasi huko Alexandria, Misri na Wazayuni 6 waliuawa kwa kupigwa risasi hiyo.  

Wakati huo huo vyombo vya habari vimeripoti kuwa, polisi aliyefanya mauaji hayo ametiwa mbaroni. Ufyatuaji risasi huu tajwa dhidi ya watalii wa Kizayuni umejiri  siku moja baada ya kuanza operesheni ya mafanikio ya muqawama wa Palestina (Kimbunga cha Al Aqsa) dhidi ya utawala wa Kizayuni. 

Wanamuqwama wa Palestina 

Wanamapambano wa Palestina tangu jana asubuhi Jumamosi wameanza operesheni yao ya pande zote na ya kipekee kwa jina la Al-Aqsa Storm yaani Kimbunga cha Al Aqsa kutokea Gaza wakipinga sera za kujitanua za utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. 

Oparesheni hii ya pande zote na tata ya muqawama wa Palestina ambayo imetekelezwa kupitia njia za chini ya ardhi,baharini na angani pamoja na kuvurumisha maelfu ya maroketi na makombora katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) hadi sasa imepelekea kuuliwa Wazayuni wasiopungua 350 na kujeruhiwa wengine zaidi ya 1,800.  

Kutekwa zaidi ya askari mia moja wa Kizayuni akiwemo meja Jenerali wa utawala huo na kudhibitiwa kwa muda vitongoji saba vya walowezi wa Kizayuni ni miongoni mwa mafanikio mengine ya operesheni hiyo ya kipekee ya muqawama wa Palestina.