Brigedi za Qassam zatungua helikopta ya Israel Ukanda wa Gaza
Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza habari ya kufanikiwa kutungua helikopta ya utawala haramu wa Israel, ikiwa ni kuendelea kujibu jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Taarifa iliyotolewa leo Alkhamisi na Izzuddin Qassam imesema, vikosi vyake katika siku ya 20 ya Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa vimefanikiwa kutungua helikopta ya Wazayuni kwa kutumia kombora la SAM-7, mashariki mwa kambi ya wakimbizi ya Bureij katika Ukanda wa Gaza.
Mapema leo, vyombo vya habari vya Palestina viliripoti kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeshambulia kambi ya wakimbizi ya Bureij katika Ukanda wa Gaza kwa kutumia mizinga na maroketi yanayovurumishwa kutoka kwenye vifaru.
Hata hivyo Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimejijibu chokochoko hizo kwa kutungua helikopta ya Wazayuni.
Siku chache zilizopita pia, makomandoo wa kikosi maalum cha Marekani na Israel waliangamizwa na wanamapambano wa HAMAS walipojaribu kupenya na kuingia katika Ukanda wa Gaza ili kubaini eneo wanaloshikiliwa mateka wa Israel.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limekiri kwamba, askari zaidi ya 307 wa utawala huo wameuawa tangu kuanza kwa Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa mnamo Oktoba 7.
Aidha operesheni hiyo hadi sasa imepelekea kuangamizwa Wazayuni wasiopungua 1,500 na kujeruhiwa wengine karibu 5,000, mbali na mamia ya wengine kukamatwa mateka na wapigania uhuru wa Palestina.