Sayyid Hassan Nasrullah: Kushindwa kwa adui Mzayuni hakuna shaka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105152-sayyid_hassan_nasrullah_kushindwa_kwa_adui_mzayuni_hakuna_shaka
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza utayarifu kamili wa muqawama katika nyanja mbalimbali na kuutaja ushindi wa mwisho wa muqawama na kushindwa adui Mzayuni kkwamba, ni hakika na jambo lisilo la shaka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 23, 2023 11:04 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrullah: Kushindwa kwa adui Mzayuni hakuna shaka

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza utayarifu kamili wa muqawama katika nyanja mbalimbali na kuutaja ushindi wa mwisho wa muqawama na kushindwa adui Mzayuni kkwamba, ni hakika na jambo lisilo la shaka.

Samahat Sayyyid Hassan Nasrullah amesema hayo mjini Beirut Lebanon katika mazungumzo yake na Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kkusisitiza kwamba, ushindi ni wa muqawana na bila shaka adui atashindwa.

Katika mazungumzo hao wawili hao wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na matukio ya hivi punde katika eneo, Lebanon na Palestina na vita vya Gaza na wajibu wa pande zote katika kipindi hiki cha kihistoria na cha hatima ni kuunga mkono suala la Palestina na Quds takatifu na juhudi za sasa za kisiasa za kusimamisha mashambulio ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akiwa katika mazungumzo na Najib Miqati Waziri Mkuu wa Lebanon

 

Katika kikao hicho, Waziri wa Mashauri ya kkigeni wa Iran  alimfahamisha kwa kifupi kuhusu harakati na mashauriano ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wiki zilizopita kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Palestina na kukomesha jinai za kivita za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza.

Kwa upande wake Samahat Seyyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria pia kusimama kidete kusiko na mithili kwa wapiganaji wa muqawama na wananchi wanamuqawama wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza utayarifu kamili wa muqawama katika nyanja mbalimbali na kusisitiza kwamba, kambi ya muqawama itapata na kushindwa kwa adui wa Kizayuni ndio uhalisia na jambo lisilo na shaka.