Hizbullah yaendelea kuishambulia Israel, yaangamiza idadi kubwa ya wanajeshi Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105160-hizbullah_yaendelea_kuishambulia_israel_yaangamiza_idadi_kubwa_ya_wanajeshi_wazayuni
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon jana Alkhamisi ilitoa taarifa 10 za mfululizo na kutangaza kuwa, imeyapiga kwa makombora maeneo hassas na muhimu ya adui Mzayuni na kuangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 23, 2023 23:21 UTC
  • Hizbullah yaendelea kuishambulia Israel, yaangamiza idadi kubwa ya wanajeshi Wazayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon jana Alkhamisi ilitoa taarifa 10 za mfululizo na kutangaza kuwa, imeyapiga kwa makombora maeneo hassas na muhimu ya adui Mzayuni na kuangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa Israel.

Shirika la habari la Tasnim limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon inaendelea kuwasaidia na kuwaunga mkono ndugu zao Wapalestina kupitia kulipiza kisasi cha jinai za Israel katika Ukanda wa Ghaza. Hizbullah inaendelea kuyapiga kwa makombora maeneo muhimu ya kijeshi ya adui Mzayuni.

Katika moja ya taarifa zake hizo za mfululizo ilizozitoa jana asubuhi, Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, inaendelea kuunga mkono mapambano ya kishujaa ya wananchi wa Ghaza na ndio maana Alkhamisi tarehe 23 Novemba, 2023, saa mbili na nusu asubuhi kwa majira ya eneo hilo, imewashambulia wanajeshi wa Israel katika eneo la al Zahir na kuwasababishia hasara kubwa. 

Wanajeshi Wazayuni wakihesabu maiti wao

 

Taarifa nyingine ya Hizbullah ya Lebanon imesema, jana saa hiyo hiyo mbili na nusu asubuhi ilishambulia kundi jingine la wanajeshi wa Israel katika eneo la Jal al Ulam (جل العلام) na kuwasabishia maafa makubwa Wazayuni hao. 

Taarifa ya tatu ya Hizbullah ya Lebanon iliyotolewa jana asubuhi imesema kuwa, wanamapambano wa Hizbullah wamewashambulia kwa silaha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika eneo la Barka Risha na kuwatia hasara kubwa. 

Kwa mujibu wa taarifa hizo 10 zilizotolewa mfululizo na Hizbullah ya Lebanon jana Alkhamisi asubuhi, wanamapambano hao wa Lebanon wamewasababishia wanajeshi Wazayuni hasara kubwa za roho na vifaa vya kijeshi ikiwa ni kulipiza kisasi cha kuuliwa shahidi wanamapambano watano wa Hizbullah usiku wa kuamkia jana Alkhamisi katika maeneo ya mpakani mwa Lebano na kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.