Sisitizo la UNICEF la kufikiwa usitishaji vita wa kudumu Gaza
James Elder, Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) sambamba na kusisitiza kufikiwa usitishaji vita wa kudumu huko Gaza, amesema kuwa kitendo cha kushambuliwa kwa mabomu watoto huko Gaza hakipaswi kurudiwa tena.
Kwa mujibu wa IRNA; James Elder alisema katika mahojiano na Kanali ya Ufaransa 24 Jumapili kwamba: Usitishaji vita wa siku nne kati ya Israel na Hamas umetupa fursa ambayo hatukuwa nayo mwezi mmoja uliopita ya kufikisha misaada zaidi huko Gaza.
Alisisitiza kwamba: Misaada hii haipaswi kukomeshwa katika siku mbili zijazo na watoto wa Kipalestina kushambuliwa tena kwa mabomu.
Ameendelea kusema: Tunahitaji usitishaji vita wa kudumu, vinginevyo tutaendelea kushuhudia tu uharibifu na vifo vya watoto.
Kwa kupita zaidi ya siku 40 za mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa zaidi ya watoto 800 wameuawa shahidi na wengine 2,450 kujeruhiwa katika vita vya Gaza.
Shirika hilo limesema maelfu ya watoto wa Kipalestina wanahitaji misaada ya kibinadamu huku wakiendelea kuteseka na matokeo mabaya ya vita vya kikatili vya Isreal katika eneo hilo.