Makumi ya wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa na kujeruhiwa kaskazini mwa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106440-makumi_ya_wanajeshi_wa_kizayuni_waangamizwa_na_kujeruhiwa_kaskazini_mwa_gaza
Wanajeshi 40 wa Kizayuni wameangamizwa au kujeruhiwa katika operesheni iliyotekelezwa jana Jumatatu na Brigedi za Izzuddinul Qassam tawi la kijeshi la Hamas huko Jabalia, kaskazini mwa Ghaza.
(last modified 2023-12-26T03:09:50+00:00 )
Dec 26, 2023 03:09 UTC
  • Makumi ya wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa na kujeruhiwa kaskazini mwa Gaza

Wanajeshi 40 wa Kizayuni wameangamizwa au kujeruhiwa katika operesheni iliyotekelezwa jana Jumatatu na Brigedi za Izzuddinul Qassam tawi la kijeshi la Hamas huko Jabalia, kaskazini mwa Ghaza.

Brigedi za Izzuddinul Qassam zililenga kwa maroketi ya TBG kundi la askari vamizi 40 wa Israel waliokuwa ndani ya jengo moja mjini Jabalia na kuwaua au kuwajeruhi.

Vikosi vya Qassam pia vilifanikiwa kuharibu na kuteketeza kwa maroketi ya Yasin 105 magari 9 ya kivita ya utawala wa Kizayuni yalipojaribu kupenya katika vitongoji 2 vya Tafah na Al-Darj katika mji wa Gaza.

Vikosi vya Al Qassam vilitangaza mapema katika taarifa yake kwamba vililipua bomu na kuua kundi la wavamizi walioingia chini ya ardhi katika eneo la Khaza'ah huko Khan Yunis.

Wapiganaji wa Hamas wakirusha rocketi ya Tandem

Brigedi za Izzuddinul-Qassam pia zimesisitiza kuwa zimelenga mabulldoza ya wavamizi katika eneo la Khan Yunis kwa maroketi ya Tandem.

Tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala unaoikalia kwa mabavu  Quds, na  ili kulipiza kisasi na kufidia kushindwa kwake na kukomesha operesheni za makundi ya Kipalestina, utawala huo umekuwa ukishambulia kinyama maeneo ya makazi, matibabu na kitamaduni ya Ukanda wa Gaza.