Upinzani dhidi ya Netanyahu washadidi kwa kushindwa kwenye vita vya Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i107006-upinzani_dhidi_ya_netanyahu_washadidi_kwa_kushindwa_kwenye_vita_vya_ghaza
Matokeo ya uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni yaliyotangazwa leo Jumanne yanaonesha kuwa, upinzani dhidi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, umeongezeka sana kutokana na kufeli katika vita vya Ghaza.
(last modified 2024-01-09T08:17:22+00:00 )
Jan 09, 2024 08:17 UTC
  • Upinzani dhidi ya Netanyahu washadidi kwa kushindwa kwenye vita vya Ghaza

Matokeo ya uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni yaliyotangazwa leo Jumanne yanaonesha kuwa, upinzani dhidi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, umeongezeka sana kutokana na kufeli katika vita vya Ghaza.

Shirika la habari la Mehr limetangaza habari hiyo na kusema kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya karibuni kabisa wa maoni, umaarufu wa Netanyahu umeporomoka kwa asilimia 64 kutokana na kushindwa vibaya katika kuendesha na kusimamia vita vya Ghaza ambavyo ndivyo vita vilivyochukua muda mrefu zaidi katika historia ya utawala wa Kizayuni na mpaka hivi sasa umeshindwa kufanikisha lengo lake japo moja. 

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya maoni, asilimia 25 tu ya walioshiriki kwenye uchunguzi huo wamesema wanakubali Netanyahu aendelee kuwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Sehemu nyingine ya uchunguzi huo wa maoni inasema kuwa, lau kama uchaguzi utafanyika hivi sasa, chama cha Benny Gantz cha Umoja wa Kitaifa (National Unity), kitapata viti 33, na chama cha Likud cha Benjamin Netanyahu kitapata viti 20 tu. 

Hii ni katika hali ambayo chama cha Gantz kilipata viti 12 tu kwenye uchaguzi uliopita na chama cha Likud cha Benjamin Netanyahu kilipata viti 33.

Uchunguzi huo wa maoni unaonesha pia kuwa, asilimia 55 ya wakati wa utawala wa Kizayuni wanaunga mkono uamuzi wa mkuu wa jeshi la utawala wa Kizayuni, Herzi Halevi, wa kuunda kamati ya kuchunguza ni kwa nini Israel ilishindwa kuzuia operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa iliyoendeshwa na wanamapambano wa Palestina tarehe 7 Oktoba, 2023.

Operesheni hiyo iliyoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilitoa pigo kubwa la kisiasa, kiusalama, kijeshi na kiintelijinsia kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.