Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa na muqawama yafika 522
Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kuwa, idadi ya askari wake waliouawa hadi sasa tangu ilipototekelezwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa imefikia 522.
Taarifa ya jeshi la Israel iliyotolewa usiku wa kuamkia leo imeeleza kuwa, askari mwingine wa jeshii hilo mwenye umrii wa miaka 21 ameuawa na wanamapambano wa HAMAS kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, askari wengine kadhaa wa jeshi la Israel wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, idadi ya askari wa Israel waliouawa ni zaidi ya hiyo hasa kutokana na mamlaka husika kutotoa takwimu sahihi.
Utawala dhalimu wa Israel ambao umeshindwa kwenye medani za mapambano, umeamua kumalizia hamaki zake kwa kuua watoto wadogo, wanawake, vizee na raia wa kawaida huko Gaza.
w
Katika upande mwingine, imeelezwa kuwa, wakati mfumo wa afya ya akili wa Israel unakabiliwa na hatari ya kuporomoka, madaktari wa magonjwa ya akili wanaondoka kuelekea Uingereza kutafuta hali bora zaidi ya maisha.
Kugura huko kwa madaktari wa afya ya akili kunakuja wakati mahitaji ya huduma za afya ya akili huko Israel yanaongezeka kutokana na vita vya Gaza, na kwamba wiki iliyopita wakuu wa vituo vya afya ya akili walituma barua kwa Mdhibiti wa Serikali, Matanyahu Englman, wakionya kwamba "mfumo wa afya ya akili wa Israel unakaribia kusambaratika kabisa.”
Tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala unaoikalia kwa mabavu Quds, na ili kulipiza kisasi na kufidia kushindwa kwake na kukomesha operesheni za makundi ya Kipalestina, utawala huo umekuwa ukishambulia kinyama maeneo ya makazi, matibabu na kitamaduni ya Ukanda wa Gaza.