ZDF yaikosoa Israel kwa kuwafunza watoto jinsi ya kuwaua Wapalestina
Televisheni ya Ujerumani ya ZDF imeonesha filamu inayoukosoa utawala haramu wa Isarel kwa kuwafundisha watoto mashuleni chuki na jinsi ya kuwadhalilisha na kuwaua Wapalestina.
Filamu hiyo inasema shule za Israel zinawafunza watoto jinsi ya kuwaua na kuwadhalilisha Wapalestina. Vilevile inaashiria jinsi vitabu vya wanafunzi katika shule za Israel vinavyotumika kuwafunza watoto chuki na vinyongo dhidi ya Wapalestina na vilevile mafundisho ya kibaguzi.
Hii si mara ya kwanza kwa televisheni za Ujerumani kuonesha filamu za matukio ya kweli (documentary) zinazofichua mafundisho ya kibaguzi katika shule za Israel.
Mwaka 2014 pia vyombo vya habari vya Ujerumani vilikosoa vikali mashambulizi na mauaji yaliyokuwa yakifanywa na jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.