Jun 24, 2024 06:52 UTC
  • Wakazi wa utawala wa Kizayuni waitisha mgomo mkubwa hadi Netanyahu aanguke

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limetangaza habari ya kuitishwa mgomo mkubwa zaidi wa maeneo yote ya utawala wa Kizayuni hadi serikali ya Benjamin Netanyahu itakapopigwa na chini.

Baada ya kupita miezi minane ya mashambulizi ya kikatili dhidi ya Ghaza bila ya kufikiwa hata lengo moja lililotangazwa na Netanyahu, hivi sasa migogoro ya ndani na nje ya Israel imeongezeka na wakazi wa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel wamechoshwa na uongo wa Netanyahu na genge lake na sasa wameamua kuanzisha mgomo mkubwa zaidi hadi itakaposambaratishwa serikali hiyo ya Wazayuni wenye misiamamo ya kufurutu ada. 

Gazeti hio la Kizayuni limeandika katika toleo lake la jana kwamba, viongozi wa upinzani wameitisha mgomo mkubwa wa kona zote dhidi ya Benjamin Netanyahu na genge lake la mawaziri wenye misimamo mikali kupindukia.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, mgomo mkubwa zaidi utaanza tarehe 7 mwezi ujao wa Julai na utaendelea hadi bunge la Knesset livunjwe na serikali ya Netanyahu isambaratishwe. 

Operesheni ya kishujaa ya Kimbunga cha al Aqsa iliyoongozwa na harakati ya HAMAS tarehe 7 Oktoba 2023 imeongeza mizozo mikubwa baina ya viongozi wa utawala wa Kizayuni na hivi sasa viongozi hao wanakulana nyama, kila mmoja anamtupia lawama mwenzake kwa kushindwa katika vita vya Ghaza na kushindwa kuzuia operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa.