Wanajeshi 70 wa Israel waangamizwa katika shambulio la ardhini Lebanon
(last modified Fri, 25 Oct 2024 02:40:00 GMT )
Oct 25, 2024 02:40 UTC
  • Wanajeshi 70 wa Israel waangamizwa katika shambulio la ardhini Lebanon

Zaidi ya wanajeshi 70 wa Israel wameangamizwa na askari na maafisa zaidi ya 600 wamejeruhiwa katika shambulio la ardhini la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel huko Lebanon.

Wapiganaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon wameharibu vifaru 28 vya Merkava, tingatinga 4, gari moja la kivita na ndege kadhaa zisizo na rubani na zenye rubani.

Ripoti zinaeleza kuwa, jeshi la utawala ghasibu wa Israel limepata hasara kubwa katikak vita vya ardhiini huko Lebanon.Taarifa zaidi ziinasema kuuwa, wanajeshi wengine wengi wamejeruhiwa huku baadhi yao wakiwa mahututi, wakati wa makabiliano hayo yaliyofuatia mashambulizi ya kuvizia ya Hizbullah, na kuongeza kwamba kuna udhibiti mkali uliowekwa na jeshi la Israel karibu na eneo yalipojiri mapigano hayo.

Wakati huo huo, wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon wameshambulia kwa makombora kadhaa viwanja vya ndege vya Ben Gurion na Ramat David katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni yaliyopachikwa jina bandia la Israel.

Siku ya Jumanne Hizbullah iliweka rekodi ya kutekeleza operesheni 39 katika muda wa siku moja kulenga ngome, vikosi, shabaha, zana za kivita, vitongoji, na kambi za utawala wa Kizayuni katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) na kusini mwa Lebanon.Hizbullah ya Lebanon haijanyamazia kimya jinai za utawala wa Kizayuni za kuwalenga raia wa nchi hiyo na tangu wakati huo imeshatekeleza operesheni kadhaa za mashmbulio dhidi ya ngome na vituo vya utawala wa Kizayuni.

Tags