Mashambulio ya Hizbullah ya Lebanon katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
(last modified Thu, 18 Jul 2024 09:38:42 GMT )
Jul 18, 2024 09:38 UTC
  • Mashambulio ya Hizbullah ya Lebanon katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imetangaza kufanya shambulio la makombora katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Katika saa 24 zilizopita, Hizbullah imelenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel huko Palestina mara tatu kwa makombora 80.

Radio ya Jeshi la utawala katili wa Israel pia imeripoti kwamba makombora ya Hizbullah yamerushwa katika maeneo ya Nahariya na Miron kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Shambulio la Hizbullah dhidi ya makazi ya Wazayuni 

Ving'ora vya hatari ya kurushwa makombora vilisikika huko Nahariya, ambapo walowezi zaidi ya 60,000 wa Kizayuni walikimbilia kwenye maficho ya chini ya ardhi ili kulinda usalama wao.

Vyombo vya habari vya utawala huo katili pia vimechapisha ripoti zinazoonyesha kushangazwa kwao na kasi ya mashambulizi yanayofanywa na Hizbullah katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel huko Palestina.

Kanali ya televisheni ya Al-Jazeera pia iliripoti Jumatano usiku kuhusu kushtushwa vyombo vya habari vya Wazayuni na ongezeko la mashambulizi ya makombora ya Hizbullah katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel huko Palestina katika siku za karibuni.

Katika miezi michache iliyopita na kufuatia jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika eneo hilo, Hizbullah ya Lebanon imekuwa ikilenga maeneo ya kijeshi ya utawala huo kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel), suala ambalo limeibua hofu na woga mkubwa kwa Wazayuni wanaoishi katika maeneo hayo.

Hadi sasa makumi ya maelfu ya Wazayuni wamekimbia vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi karibu na mipaka ya Lebanon kwa hofu ya kushambuliwa na muqawama.

Tags