Sep 10, 2024 02:25 UTC
  • Kusikika mayowe ya kuunga mkono Palestina barani Ulaya na Marekani

Mjini London, Paris, Berlin, Geneva, Milan, The Hague, Stockholm, Amsterdam, Oslo na New York, ilishuhudia waandamanaji wakipiga nara dhidi ya utawala katili wa Israel kuunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Mjini London, waandamanaji wa mataifa na dini mbalimbali wakiwa wamebeba bendera ya Palestina, waliimba nara za kudai haki, mwisho wa mfumo wa ubaguzi wa rangi, kusimamisha vita mara moja, na kupaza sauti wakisema: "Komesha uvamizi" na "Iacheni Palestine iwe Huru." Waandamanaji kwanza walikusanyika katika eneo karibu na Kasri ya Kifalme wa Uingereza na huku wakitangaza mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina, waliandamana kuelekea kwenye ubalozi wa serikali bandia ya Israel. Aidha walitoa mwito wa Israel kuwekewa vikwazo vya silaha.

Serikali ya Uingereza ya chama cha Labour inaamini katika kubadilisha mbinu katika mahusiano na Israel na imetangaza kufuta baadhi ya leseni za kuuziwa silaha Israel. Lakini wataalamu wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa hii ni hatua ya kimbinu na hatupaswi kusubiri mabadiliko makubwa katika uhusiano wa Uingereza na Israel.

Kimsingi, hakuna tofauti ya kimaoni kati ya wahafidhina na Chama cha Labour katika kuunga mkono utawala wa Kizayuni. "Iqbal Mohammad", mmoja wa wawakilishi huru wa Bunge la Uingereza na muungaji wa Palestina, alishiriki katika maandamano dhidi ya Israel huko London ambapo alisema uamuzi wa Uingereza wa kufuta uidhinishaji wa mikataba 30 kati ya 350 ya silaha na Utawala wa Kizayuni na na kuchukua uamuzi kuanzisha tena msaada wa kifedha kwa UNRWA ni kama "tone la maji kwenye bahari".

 

Na aliendelea kusema kuwa; "Mimi ni mbunge, lakini hili ni tone la bahari na tunahitaji kufanya zaidi. Kwa maana kwamba, tunahitaji kuongeza juhudi zaidi za kuwaunga mkono wananchi wa Palestina kwa nguvu zote.

Mabadiliko ya mielekeo ya kisiasa na kipropaganda ya serikali za Ulaya kuhusiana na utawala wa Kizayuni ni mabadiliko makubwa katika uhusiano wa Israel na waitifaki wake wa kistratijia wa Ulaya na Marekani. Wakuu wa serikali za Ulaya akiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Rishi Sonak, walikwenda Tel Aviv baada ya operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa na kutangaza uungaji mkono wao kamili kwa mashambulizi ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na kuangamizwa muqawama wa Kiislamu wa Palestina.

Zikiwa na lengo la kuuunga mkono utawala wa Kizayuni, serikali za Ulaya hazikuishia kutoa misaada hiyo tu bali zilikuwa zikifuatilia kuhakikisha kuwa, kuwaunga mkono Wapalestina kunatambuliwa kuwa ni kosa la jinai na kupiga marufuku kubeba bendera ya Palestina na nembo yoyote ya Palestina. Sasa hivi ikiwa uunakariibia kuingia mwaka mmoja wa uvamizi wa Wazayuni katika Ukanda wa Gaza, anga ya kisiasa dhidi ya utawala wa Israel ilizitia kivuli nchi za Ulaya na Marekani kiasi kwamba serikali za Ulaya zinaonyesha kuwa ni waungaji mkono wa amani na mazungumzo kuhusu kusitisha vita huko Ukanda wa Gaza.

Maandamano ya kuunga mkono Palestina huko nchini Norway

 

Baada ya uvamizi wa Wazayuni katika Ukanda wa Gaza uliofanywa kwa ajili ya kukabiliana na operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa, kambi mpya ilianziishwa dhidi ya utawala wa Kizayuni, nayo ilikuwa ni kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina katika nchi za Magharibi. Katika kipindi chote tangu kuanzishwa kwa dola bandia la Israel katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, sauti ya watu wa Palestina haijawahi kusikika katika fikra za umma duniani kama ilivyo hivi sasa.

Huku jinai za Wazayuni zikiendelea katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, wimbi la chuki na maandamano dhidi ya Wazayuni linazidi kupata sura mpya. Kama mpaka hadi jana mhimili wa muqawama dhidi ya utawala unaoukalia kwa mabavu Baytul- Muqaddas ulikuwa na mipaka na kuishia tu kwa harakati ya muqawama ya Kiislamu ya Palestina, Hizbullah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen, makundi ya muqawama ya Kiislamu ya Iraq na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hii leo muqawama dhidi ya Wazayuni watenda jinai na wanaoiikalia kwa mabavu Palestina hautambui mpaka.