UN yasisitiza kuhitimishwa vita Ukanda wa Gaza na Lebanon
Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Syria ametaka kuhitimishwa vita katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Geir Pedersen ambaye alitembelea mji mkuu wa Syria, Damascus amesisitiza kuhusu kuhitimishwa vita huko Lebanon na Ukanda wa Gaza na kutoiingiza Syria katika mizozo ya kikanda na kueleza kuwa kuna udharura wa kuhitimisha vita huko Lebanon na Gaza.
Kabla ya mazungumzo na Bassam al Sabagh Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria; Pedersen alibainisha kuwa: Ni muhimu kuhakikisha usitishaji vita wa haraka katika Ukanda wa Gaza naLebanon unafanyika pasina na kuitumbukiza Syria katika mizozo ya kikanda.
Mjumbe Maalumu wa Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza haya katika hali ambayo utawala bandia wa Kizayuni hadi sasa umeishambulia Syria mara kadhaa tangu uanzishe vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza Oktoba7 mwaka jana.