Gaza imeshinda: Watumiaji wa mitandao ya kijamii wazungumzia usitishaji mapigano Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121508-gaza_imeshinda_watumiaji_wa_mitandao_ya_kijamii_wazungumzia_usitishaji_mapigano_gaza
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamezungumzia habari ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel katika Ukanda wa Gaza kwa hisia mchanganyiko za furaha na matumaini ya mustakbali mwema.
(last modified 2025-11-23T06:16:50+00:00 )
Jan 16, 2025 11:17 UTC
  • Gaza imeshinda: Watumiaji wa mitandao ya kijamii wazungumzia usitishaji mapigano Gaza

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamezungumzia habari ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel katika Ukanda wa Gaza kwa hisia mchanganyiko za furaha na matumaini ya mustakbali mwema.

Watumiaji wengi wanasherehekea kile wanachokiona kama ushindi wa harakati za Muqawama na mapambano ya ukombozi wa Palestina katika kampeni ya kikatili ya mauaji ya kimbari ya Israel iliyoendelea kwa miezi 15, ambao yamesababisha vifo na uharibifu mkubwa huko Gaza, gereza kubwa zaidi la wazi duniani.

"Gaza imeshinda, Palestina imeshinda, Muqawama umeshinda," ameandika mwanamke wa Kipalestina kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Mpalestina huyo aliyejitambuliisha kama Nerdeen Kiswani ameendelea kuandika kuwa: "Ubeberu na Uzayuni umeshindwa, Chama cha Democratic cha Marekani kimeshindwa, na mustakabali wa dola la Kizayuni unaendelea kumomonyoka."

Amesema kila mtu "aliyeshiriki, kusaidia na kuunga mkono mauaji haya ya kimbari ataendelea kulipa gharama." @NerdeenKiswani

Ukurasa wa X wa Nerdeen Kiswani

 

Mwandishii habari wa Middle East Eye, Yasmine El-Sabawi, amesema "alizidiwa na hisia kuwatazama Wapalestina huko Gaza wakilipuka katika afueni na furaha iliyosubiriwa kwa muda mrefu kutokana na habari za makubaliano ya kusitisha mapigano." @yasmineelsabawi

"Waliopo hii leo wamenusurika katika mauaji ya kimbari ambayo tulikuwa tukiyarusha hewani moja kwa moja kwa simu zetu za rununu kwa muda wa miezi 16, kwa sababu Israel ilikataa kuyasitisha", amesema Yasmine El-Sabawi. 

Hisia zinazohusiana na usitishaji mapigano huko Gaza pia zinajumuisha shutuma kali dhidi ya ubeberu na Uzayuni. Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamiii wanaangazia kushindwa kwa waungaji mkono wa Kimagharibi wa Israel, hususan Marekani, katika uungaji mkono wao kwa utawala huo dhalimu.

Ukurasa wa X wa Yasmine El-Sabawi

 

Rajab Abddulhaq anasema: "Makubaliano ya kusitisha mapigano yanawakilisha pigo jingine kwa ubeberu wa Marekani na mradi wa ukoloni wa walowezi wa Kizayuni. Walijaribu kufuta Muqawama kupitia mauaji ya kimbari na jinai, lakini watu wa Gaza wamesimama kidete na kuendeleza mapambano hadi pumzi ya mwisho." @Raja48

Nora Barrows, ripota na mhariri msaidizi wa The Electronic Intifada, amesema usitishaji huo wa mapigano umepatikana "kwa sababu ya ushujaa, ushupavu na werevu wa Muqawama wa Palestina, na msaada wa kibinadamu wa vikosi vya Lebanon na Yemeni."

Mwandishi wa habari Rania Khalek @RaniaKhalek anasema amefurahishwa na makubaliiano ya kusitishwa mapigano, lakini hakuna mtu anayeweza "kupumzika hadi mabeberu waliohusika na mauaji ya kimbari na kusababisha uharibifu mkubwa huko Gaza watakapowajibishwa na mifumo yao kuvunjwa."