'Uwanja wa ndege wa Ben Gurion hautakuwa salama mpaka uchokozi dhidi ya Ghaza utakapokoma'
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen (YAF) vimetangaza kuwa Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wa Israel sasa hauko salama kwa usafiri wa anga na utaendelea kuwa hivyo hadi uchokozi wa utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Ghaza utakapokomeshwa na vizuizi vya misaada lilivyoekewa eneo hilo la Palestina vitakapoondolewa.
Brigedia Jenerali Yahya Saree amebainisha kuwa, mashambulizi hayo, ni jibu kwa uchokozi unaoendelea kufanywa na Marekani dhidi ya Yemen.
Msemaji wa YAF ametoa pongezi pia kwa wananchi wa Palestina na Muqawama wao huko Ghaza, na kusifu uthabiti wao wa kuhimili hujuma za kikatili za Wazayuni.
Operesheni mpya za Yemen dhidi ya shabaha za Israel na Marekani zimeanza tena baada ya utawala wa Kizayuni kuvunja makubaliano ya usitshaji vita yaliyodumu kwa miezi miwili huko Ghaza, ambayo yalifikiwa baina yake na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas.
Shambulio la makombora la Yemen la leo Ijumaa ni operesheni ya nne kutekelezwa katika wiki hii kulenga maeneo ya kati ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina bandia la Israel baaada ya utawala huo wa Kizayuni kuanza tena kufanya mauaji ya kimbari huko Ghaza.../