Mamilioni ya Waisraeli wajificha kwenye mahandaki baada ya kombora la Yemen kulenga uwanja wa ndege
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i130120-mamilioni_ya_waisraeli_wajificha_kwenye_mahandaki_baada_ya_kombora_la_yemen_kulenga_uwanja_wa_ndege
Jeshi la Yemen limefanikiwa tena kulenga Ben Gurion, uwanja mkubwa wa ndege wa utawala wa Israel, katika operesheni mpya ya kuunga mkono Wapalestina ambayo ilisababisha makaazi ya walowezi haramu kukimbilia kwenye mahandaki huku wakiwa na hofu na wahka.
(last modified 2025-08-28T11:36:08+00:00 )
Aug 28, 2025 11:36 UTC
  • Mamilioni ya Waisraeli wajificha kwenye mahandaki baada ya kombora la Yemen kulenga uwanja wa ndege

Jeshi la Yemen limefanikiwa tena kulenga Ben Gurion, uwanja mkubwa wa ndege wa utawala wa Israel, katika operesheni mpya ya kuunga mkono Wapalestina ambayo ilisababisha makaazi ya walowezi haramu kukimbilia kwenye mahandaki huku wakiwa na hofu na wahka.

Tukio hili lilitokea Jumatano, ambapo majeshi yalithibitisha kulipua kituo hicho kwa kombora la "Palestine-2" la balistiki. 

Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa uwanja wa ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv umelengwa kwa shambulio la kombora la balestiki la nchi hiyo.

Siku ya Jumatano, Brigedia Jenerali Yahya Saree alitangaza operesheni maalum ya kijeshi ya kulenga Uwanja wa Ndege wa Ben-Gurion kwa kombora la masafa marefu la "Palestina 2" na kusema kuwa operesheni hiyo ilifanikiwa na kupelekea mamilioni ya Wazayuni kukimbilia kwenye mahandaki na kusimamisha operesheni za kawaida za uwanja huo wa ndege.

Akisisitiza kuwa operesheni hiyo ilifanywa kwa ajili ya kulisaidia taifa linalodhulumiwa la Palestina na Mujahidina wake na katika kukabiliana na jinai za mauaji ya halaiki na njaa zinazofanywa na adui wa wakazi wa Gaza, msemaji huyo wa jeshi la Yemen ameongeza kuwa, kutambuliwa duniani kote ukubwa wa mateso ya watu wa Gaza ikiwemo njaa, mzingiro na uchokozi, kunayawajibisha kihistoria mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.  Jenerali

Yahya Saree ametoa wito kwa Umma wa Kiarabu na Kiislamu, ambao una wajibu wa kidini, kiutu na kimaadili, kuchukua hatua za kukomesha njaa, kuondoa mzingiro na kusimamisha mashambulizi ya kichokozi ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.

Jeshi la Yemen limetekeleza mamia ya operesheni katika kuonyesha mshikamano na wakazi wa Ukanda wa Gaza tangu Israel ilipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo Oktoba 7, 2023. Tangu wakati huo utawala wa Kizayuni umeshadidisha jinai na mashambulizi ya kikatili ambayo hadi sasa yamesaabisha kuuliwa shahidi Wapalestina zaidi ya 64,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.