Je, Israel inakabiliwa na "Hatima ya Afrika Kusini"?
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i131058-je_israel_inakabiliwa_na_hatima_ya_afrika_kusini
Tovuti ya Kiingereza ya BBC katikati ya Septemba 2025 katika makala ya kina yenye kichwa cha habari kilichosomeka "Je, Israel Inakabiliwa na 'Hatima ya Afrika Kusini'?" Ilizungumzia suala la kujikariri uzoefu wa Afrika Kusini kwa utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2025-09-21T06:03:03+00:00 )
Sep 21, 2025 06:03 UTC
  • Je, Israel inakabiliwa na

Tovuti ya Kiingereza ya BBC katikati ya Septemba 2025 katika makala ya kina yenye kichwa cha habari kilichosomeka "Je, Israel Inakabiliwa na 'Hatima ya Afrika Kusini'?" Ilizungumzia suala la kujikariri uzoefu wa Afrika Kusini kwa utawala ghasibu wa Israel.

Pamoja na kuendelea kwa vita vya Gaza, Israel inazidi kukabiliwa na kutengwa kimataifa. Waangalizi wengi wanahoji kama Israel inapitia "wakati wa Afrika Kusini"; wakati vikwazo vya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo vilipoufanya utawala wa ubaguzi wa rangi kupiga magoti. Mawaziri Wakuu wa zamani wa Israel, Ehud Barak na Ehud Olmert, wameonya kuwa Netanyahu ameigeuza Israel kuwa utawala usiokubalika duniani.

Mashinikizo ya kisheria na kidiplomasia

Kufuatia kutolewa hati ya kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, safari za kimataifa za Netanyahu zimebanwa sana. Wakati huo huo, nchi kama Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Canada na Australia zimetangaza kuwa zinakusudia kuitambua Palestina kama taifa huru.

Katika ulimwengu wa Kiarabu, hasira imeongezeka kutokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya viongozi wa Hamas nchini Qatar, na mikutano imefanyika mjini Doha kwa ajili ya kutoa jibu la pamoja kwa uchokozi huo.

Vikwazo na hatua za kiuchumi

- Ubelgiji imepiga marufuku uagizaji wa bidhaa zinazozalishwa katika maeneo ya vitongoji haramu vilivyojengwa katika Ukingo wa Magharibi Mto Jordan, kuzuia ushirikiano na mashirika ya Israeli na kuwawekea vikwazo mawaziri wenye misimamo mikali wa baraza la mawaziri la Nretanyahu.

- Uhispania imegeuza vikwazo visivyo rasmi vya silaha kuwa sheria, kupiga marufuku kuingia nchini humo watu wanaohusika katika jinai za kivita za Israel, na kuzuia utiaji nanga wa meli zinazobeba silaha kwa ajili ya utawala wa Kizayuni.

- Norway: Mfuko mkubwa zaidi wa uwekezaji duniani, wa dola trilioni 2 umesimamisha uwekezaji katika makampuni ya Israel.

- Umoja wa Ulaya unapanga kuwawekea vikwazo mawaziri wenye misimamo mikali na kusimamisha baadhi ya makubaliano ya kibiashara na Israel. Mkuu wa Tume ya Ulaya ametangaza kwamba matukio ya Gaza yametikisa "dhamiri ya ulimwengu".

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni

Upande wa utamaduni na michezo wa vikwazo

- Eurovision: Nchi za Ireland, Uhispania, Uholanzi na Slovenia zimetishia kujiondoa kwenye shindano hili la muziki ikiwa Israel itashiriki mwaka 2026.

- Sinema na sanaa: Zaidi ya wasanii 4,000, wakiwemo nyota kama Emma Stone na Javier Bardem, wametoa wito wa kususiwa matamasha na mashirika ya filamu ya Israel.

- Michezo: Mashindano ya baiskeli ya "Vuelta a España" yalitatizwa mara kadhaa na maandamano ya waungaji mkono wa Palestina ambapo sehemu ya kufanyika sherehe ya kufunga mashindano hayo ilighairiwa. Katika chess, wachezaji wa Israel walilazimika kujiondoa kwenye mashindano.

Wasiwasi kati ya wanadiplomasia wa zamani

- Jeremy Issakarov, balozi wa zamani wa utawala wa Kizayuni nchini Ujerumani, anaamini kwamba itibari ya kimataifa ya Israel imepungua sana, na kwamba baadhi ya hatua za kimataifa zinawalenga Waisrael wote na zinaweza kuwa na athari mbaya kwao.

- Ilan Baruch, balozi wa zamani wa utawala wa Kizayuni nchini Afrika Kusini, anasisitiza kuwa mashinikizo na vikwazo ni jambo la lazima na kwamba ni kwa njia hii pekee ndipo Israel italazimika kubadilisha siasa zake. Anasema yuko tayari kulipa gharama ya mashinikizo haya.

muhtasari

Israel hivi sasa inakabiliwa na wimbi la mashinikizo ya kidiplomasia, kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo ambayo wengi wanayaona kuwa sawa na mchakato uliopelekea kuporomoka utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini.

Ijapokuwa uungaji mkono wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya bado unahesabiwa kuwa ngao ya ulinzi kwa Israel, kuendelea vita huko Gaza, ongezeko la vifo vya binadamu na siasa za mrengo mkali wa kulia mjini Tel Aviv kumeongeza hatari ya Israel kuwa "utawala usiokubalika".

Siku zijazo bila shaka zitathibitisha iwapo mashinikizo haya yanaweza kuleta mabadiliko ya kimuundo katika sera za Israel kama ilivyofanyika huko Afrika Kusini au la. Pamoja na hayo, jambo lililo wazo ni kuwa: Israel haiwezi tena kudumisha msimamo wake wa awali katika jamii ya kimataifa, na hatimaye italazimika tu kubadili mkondo wake.