Israel yakiuka usitishaji vita, yaua Wapalestina 10 kila siku
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Euro-Mediterania lilitangaza siku ya Ijumaa katika ripoti yake kuwa, utawala wa Kizayuni umekuwa ukiwaua shahidi Wapalestina 10 kila siku tangu kuanza kwa usitishaji vita.
Shirika hilo lilitangaza siku ya Ijumaa katika ripoti yake kwamba, tangu kuanza kwa usitishaji vita huko Gaza tarehe 10 Oktoba, utawala wa Kizayuni kwa wastani umekuwa ukiua Wapalestina 10 kwa siku.
Kwa mujibu wa takwimu hizi, tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, vikosi vya kijeshi vya utawala huo vimewauwa shahidi Wapalestina 219, wakiwemo watoto 85. Pia, katika kipindi hiki, karibu watu wengine 600 wamejeruhiwa.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unakiuka wazi mapatano ya usitishaji vita na kutekeleza jinai na mauaji hayo ya kutisha, bila kujali lolote kwa kutambua kuwa unaungwa mkono moja kwa moja na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani.