Ndege ya kujaza mafuta ya Jeshi la Marekani imetunguliwa nchini Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i137324-ndege_ya_kujaza_mafuta_ya_jeshi_la_marekani_imetunguliwa_nchini_iraq
Makao Makuu ya Kamandi ya Kati ya Marekani (CENTCOM) yametangaza ‘kuanguka’ kwa ndege yao ya kijeshi ya kujaza mafuta angani katika eneo la magharibi mwa Iraq, na kutaja tukio hilo kuwa eti ni “ajali”. Hatahivyo Harakati ya Muqawama au Mapambano ya Kiislamu nchini Iraq imetangaza rasmi kutungua ndege hiyo ya jeshi la kigaidi la Marekani.
(last modified 2026-03-13T07:56:30+00:00 )
Mar 13, 2026 03:40 UTC
  • Ndege ya kujaza mafuta ya Jeshi la Marekani imetunguliwa nchini Iraq

Makao Makuu ya Kamandi ya Kati ya Marekani (CENTCOM) yametangaza ‘kuanguka’ kwa ndege yao ya kijeshi ya kujaza mafuta angani katika eneo la magharibi mwa Iraq, na kutaja tukio hilo kuwa eti ni “ajali”. Hatahivyo Harakati ya Muqawama au Mapambano ya Kiislamu nchini Iraq imetangaza rasmi kutungua ndege hiyo ya jeshi la kigaidi la Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya kimataifa, CENTCOM imethibitisha kwamba ndege ya aina ya KC‑135, inayotumika kwa kujaza mafuta ndege nyingine angani, imeanguka ikiwa katika anga ya Iraq.

Jeshi la Marekani pia lilidai kuwa ndege mbili zilihusika katika tukio hilo. Moja ya ndege hizo ilianguka katika eneo la magharibi mwa Iraq, ilhali ndege ya pili ilifanikiwa kutua salama. Ndege hizo za kujaza mafuta ni muhimu sana kwani hujaza mafuta ya ndege za kivita ambazo  sasa zinatumika kudondosha mabomu  nchini Iran.

Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa habari hiyo, kinyume na madai ya Jeshi la Marekani, mwandishi wa habari wa mtandao wa CBS wa Marekani aliripoti kuwa ndege hiyo ya kujaza mafuta ilitunguliwa kwa kombora kuanguka. Kwa mujibu wa taarifa yake, ndege nyingine ya kujaza mafuta pia ilipigwa, lakini iliweza kufanikiwa kutua ‘Israel’.

Kwa kuwa ndege ya kujaza mafuta ya aina hii huwa na wafanyakazi wapatao sita, inaaminika kwa uwezekano mkubwa kuwa wote waliokuwamo ndani ya ndege iliyodunguliwa wamepoteza maisha katika tukio hilo.

Msemaji wa Kamandi ya Kijeshi ya Khatam al‑Anbiya (SAW) ya Iran ametangaza kuwa ndege moja ya kujaza mafuta ya Jeshi la Marekani ilipigwa kwa kombora lililorushwa na makundi ya Muqawama katika eneo la magharibi mwa Iraq, na kuanguka, huku wafanyakazi wote waliokuwa ndani yake wakiangamia.

Wakati huo huo, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Iraq imetangaza kupitia taarifa rasmi kuwa imeidungua ndege hiyo ya kujaza mafuta ya Marekani wakati ikiwa agani katika eneo la magharibi mwa Iraq.

Harakati hiyo imesema wapiganaji wake, wakitetea mamlaka na anga ya taifa lao, waliidungua ndege hiyo katika eneo la magharibi mwa Iraq kwa kutumia kombora.