Magaidi wahamishia Israel turathi za kihistoria za Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15361-magaidi_wahamishia_israel_turathi_za_kihistoria_za_syria
Gazeti moja la Kizayuni limekiri kuwa, athari za kale zilizoibiwa nchini Syria na magaidi wanaofanya mauaji katika nchi hiyo ya Kiarabu zimepelekwa kwa wingi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 15, 2016 02:59 UTC
  • Magaidi wahamishia Israel turathi za kihistoria za Syria

Gazeti moja la Kizayuni limekiri kuwa, athari za kale zilizoibiwa nchini Syria na magaidi wanaofanya mauaji katika nchi hiyo ya Kiarabu zimepelekwa kwa wingi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika toleo lake la jana Jumatano, gazeti la Kizayuni la Haaretz liliandika ripoti na huku likiashiria kupelekwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel athari za kihistoria za Iraq baada ya kupinduliwa utawala wa kidikteta wa Saddam Husseni na kukaliwa kwa mabavu nchi hiyo ya Kiarabu, limeripoti pia kuwa athari nyingi za kihistoria za Syria nazo zinapatikana kwa wingi sana katika maduka makubwa ya Israel.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, wakati dunia ilipokuwa imeelekeza macho yake katika kulinda athari za kale za eneo la Palmyra (Tadmor)  huko Syria, picha zilizochukuliwa kwa njia ya satalaiti zinaonesha kuwa, genge la kigaidi la Daesh lilikuwa linafanya wizi mkubwa wa athari za kihistoria katika maeneo mengi ya kale ya Syria na kuzihamishia nje ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuupatia athari hizo utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakati huo huo Eitan Klein, mkurugenzi wa kitengo cha kuzuia wizi wa athari za kale katika majumba ya makumbusho ya israel naye amekiri kuwa, genge la kigaidi la ISIS linaendelea kuharibu athari za kihistoria za Syria na kuziiba na baadaye kuziua kwa bei mbaya katika masoko ya kimataifa.

Magaidi wa ISIS wanajifanya kuvunja masanamu, kumbe wanaiba athari za kihistoria na kuziua kwa bei mbaya nje ya Syria na Iraq

 

Gange la kigaidi la ISIS ni moja ya magenge makubwa ya wizi wa athari za kihistoria katika historia. Mbali na kufanya jinai za kila namna, genge la kigaidi la Daesh limeiba athari nyingi muhimu za katika maeneo ya kihisotoria ya Iraq na Syria.