Rais wa zamani wa Israel aaga dunia
Rais wa zamani wa utawala haramu wa Israel, Shimon Peres ameaga dunia usiku wa kuamkia leo, wiki mbili baada ya kupatwa na kiharusi
Kituo cha tiba cha Sheba (The Sheba Medical Center) mjini Tel Aviv kimetangaza kuwa Peres ameaga dunia tisa na dakika 40 usiku wa kuamkia leo kwa wakati wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu baada ya kukimbizwa hospitalini hapo kutokana na matatizo ya kiafya. Hali ya kiongozi huyo wa zamani wa Israel ilitangawa kuwa tata na kuingizwa moja kwa moja katika kitengo cha wagonjwa mahututi.
Katika uhai wake wa kisiasa ulioendelea kwa kipindi cha miongo saba Shimon Peres alishika nyadhifa mbalimbali katika utawala haramu wa Israel. Aliwahi kuwa Rais wa Israel, Waziri Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya utawala huo ghasibu.
Katika kipindi cha uongozi wa Shimon Peres, Wapalestina wasiopungua elfu nne waliuawa katika vita mbili tofaiti zilizoanzishwa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza kati ya mwaka 2007 na 2014.
Katika vita ya pili iliyoanza July 8, 2014 na kumalizika August 26, Wapalestina 11,100 wakiwemo watoto 3,374 na wanawake 2,088 pia walijeruhiwa.